Polisi
wakifanya kazi ya kuteketeza magunia ya Bangi.
Mamlaka ya
kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na jeshi la polisi,
wamefanya oparesheni ya kukamata na kuteketeza magunia ya bangi zaidi ya mia
tatu, Mkoani Arusha, huku ikiwakamata na kuwafungulia kesi watuhumia 18
kwa kukutwa na dawa hizo.
Katika zoezi
la uchomaji wa magunia hayo, Kamishina wa sheria mamlaka ya
kupambana na kudhibiti dawa za kulevya, Edwin Kakolaki, amesema dawa hizo ni
kutokana na msakao uliofanyika kwa nyakati mbalimbali mkoani Arusha, na
wameziteketeza kwa mujibu wa sheria namba tano ya mwaka 2015 ya ku.
Licha ya
kubainisha kupungua kwa kiwango kikubwa cha matumizi ya dawa za kulevya
hapa nchini, Kakolaki amesema baadhi ya waingizaji wamebuni mbinu mpya ya
kuingiza dawa aina ya kokeni na heroini na serikali inaendelea kuwadhibiti.
Mpaka sasa
zaidi ya waraibu 5000 wanapatiwa matibabu ili kuachana kabisa na matumizi ya
dawa za kulevya.
|
No comments:
Post a Comment