Watu 11 wafariki Baada ya Daraja Kuanguka -Colombia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 16, 2018

Watu 11 wafariki Baada ya Daraja Kuanguka -Colombia.

Watu 11 wamefariki baada ya daraja lililokuwa likijengwa na kuwajeruhi wengine watano , katika maeneo ya Chirajara kuporomoka nchini Colombia.

Maofisa wa Colombia wamesema watu waliofariki ni wafanyakazi wa Kampuni ya ujenzi ambao walikuwa kazini.

Maofisa hao wamesema wafanyakazi hao walikuwa wakishughulika na mfumo wa maji kwenye daraja wakati walipokutwa na umauti kwenye mradi huo uliopo kilomita 95 nje ya Gogota.

Picha za tukio hilo zinaonyesha eneo kubwa la daraja hilo lenye urefu wa mita 450 likiwa limeanguka. Waziri wa Usafirishaji Germán Cardona alisema chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa. 

Mfanyakazi mmoja miongoni mwa waliojeruhiwa alisimulia tukio hilo na kusema:- Kila mtu alianza kupiga kelele kuwa daraja linaanguka, sikuwa na muda wa kufanya chochote na kisha nikasikia kitu kinanipiga kichwani,”
Daraja hilo ni sehemu ya mpango mkubwa wa kuendeleza njia inayoelekea Bogota katika mbuga za mashariki ili kuifanya iwe na njia mbili. 

Kazi iliyopangwa inajumuisha ujenzi wa njia 18 za ndani ya milima, madaraja 42 pamoja na kamera za kurekodi matukio.

Njia iliyopo ambayo ni nyembamba hufungwa kila mara kutokana na malori yanayopeleka mizigo Bogota yanapoharibika na kukwamisha magari mengine kupita.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad