Ajali
iliyohusisha magari matatu huko Biharamulo, Kagera.
Watu kumi na
mmoja wamekufa na wengine watano wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari
matatu ikiwemo gari dogo la kubeba abiria na malori mawili iliyokuwa yakitokea
wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Olomi amethibitisha kutokea ajali hiyo na
tayari Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa
Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kufuatia ajali hiyo.
Ajali ambayo
imeacha simanzi kubwa miongoni mwa ndugu na familia ukiwa ni muendelezo wa
ukosefu wa umakini kwa madereva pindi wanapokuwa barabarani.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kagera, SACP Olomi amethibitisha idadi ya vifo pamoja na
majeruhi waliotokana na ajali hiyo inayodaiwa kusababishwa na mwendo kasi.
Kamanda huyo
amesema, gari hilo la abiria lilikuwa na jumla ya abiria 17 na kati ya hao 11
wamekufa na watano wameruhiwa na wanaendela kupatiwa matibabu katika hospitali
ya wilaya ya Biharamuro.
SACP Olomi
amesema, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari la abiria ambaye anadaiwa
hakutumia akili kwa kutaka kulipita gari la mbele yake bila kuwa makini na
hivyo kukutana uso kwa uso na lori .
Aidha, Mhe.
Rais Magufuli amewakumbusha watumiaji wa barabara hasa madereva kuwa makini na
kuzingatia sheria za usalama barabarani na ameviagiza vyombo vinavyohusika
kuongeza jitihada za kukabiliana na ajali za barabarani ili kuokoa maisha ya
watu na mali zinazopotea kutokana na ajali.
|
No comments:
Post a Comment