Taswira Picha 10 Yanga SC ilivyotua Dar - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 11, 2018

Taswira Picha 10 Yanga SC ilivyotua Dar

Kikosi cha klabu ya Yanga  kimewasili Dar es salaam kikitokea Viziwani Zanzibar katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuondoshwa kwenye Michuano  hiyo na Klabu ya URA ya Uganda katika nusu fainali ya kwanza, wachezaji na viongozi wa klabu hiyo wamewasili Dar es Salaam leo January 11, 2018  kutoka Mjini Unguja visiwani Zanzibar  huku wakiwa na sura za huzuni.


Chirwa akiwasili.

Yanga SC ikitolewa katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi na timu ya URA ya Uganda kwa njia ya mikwaju ya penati 5-4.

Katika mikwaju hiyo Mzambia, Obrey Chirwa alikosa bao nahivyo kuifanya URA kosanga mbele ambapo sasa atacheza mchezo wa fainali na Azam FC tarehe 13,January ,2018 siku ya Jumamosi.

Ni mara ya tatu mfululizo Yanga SC kupoteza mechi ya nusu fainali na kuaga mashindano ya Mapinduzi kwani mwaka 2016 na 2017 pia ilipoteza nusu fainali zake na kushia kuisikia fainali ya mapinduzi kwa muda mrefu.

Yanga SC wamepoteza nusu fainali kwa mara ya pili mfululizo dhidi URA na mara zote wakitolewa kwa mikwaju ya penati, mwaka 2016 walitupwa nje ya mashindano kwa penati 4-3 baada ya sare ya kufungana 1-1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad