Uongozi wa
redio Kwizera Fm umetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa iliyotolewa jana na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, na kuenea katika mitandao ya kijamii
inayomuhusisha mmoja wa waandishi wake anayetuhumiwa kujifanya afisa usalama wa
Taifa na kujipatia fedha isivyo halali kutoka kwa mganga wa jadi.
Mkurugenzi
wa Radio Kwizera, Padre Damas Missanga amesema taasisi inamtambua mtuhumiwa
huyo Bw. Saimoni Dionizi kama mwandishi wa kujitegemea anayeripotia Radio
Kwizera kutoka Kahama lakini tuhuma hizo haziihusu taasisi na wala hakutumwa
kufanya hivyo.
Padre
Missanga ameeleza kwamba Radio Kwizera, kama chombo cha habari kitaendelea
kujikita katika maadili ya uandishi wa habari wakati wote, kutoa huduma kwa
jamii kwa kuzingatia haki, weledi na sheria za nchi na hivyo inaomba radhi kwa wadau na wasikilizaji wote
waliopata usumbufu kutokana na taarifa hiyo.
Katika
taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa waandishi wa habari
watano wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya
kujifanya maafisa usalama wa taifa na kujipatia shilingi Milioni 1 kutoka kwa
Jane Mbeshi mkazi wa kitongoji cha Ng’wande kata ya Mwaluguli ambaye ni mganga wa jadi.
Waandishi
hao ni Paul Kayanda wa gazeti la Uhuru, Raymond Mihayo- Habarileo, Shaban
Njia-Jamboleo, Simon Dioniz- Radio Kwizera na George Maziku ambaye hajulikani
anaandikia chombo gani.
HAPA CHINI
ISOME TAARIFA KAMILI.
|
No comments:
Post a Comment