Taswira 21 Kumuyange FC ya Ngara ilivyouchukua Ubingwa wa Soka Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 15, 2018

Taswira 21 Kumuyange FC ya Ngara ilivyouchukua Ubingwa wa Soka Kagera.

Wachezaji wa Timu ya Kumuyange FC ya Ngara,Viongozi wa Chama cha Soka Mkoa -KRFA na Viongozi wengineo wa Chama na Serikali katika picha ya pamoja wakati Kumuyange FC wamekabidhiwa Ubingwa wa Soka mkoani Kagera 2017 /2018 baada ya kumvua Ubingwa huo Timu ya Eleven Stars ya Misenyi kwa kumfunga magoli 5-1 Jana January 14,2018 uwanjani Kaitaba,Bukoba.
Vikombe vya Ubingwa.
Mwenyekiti wa Kumuyange FC ya Ngara,Ezron Nyamunda akishangilia Ubingwa na Kombe lao.

Timu ya Kumuyange FC ya Ngara imeibuka Bingwa wa Soka mkoani Kagera 2017 /2018 baada ya kumvua Ubingwa huo Timu ya Eleven Stars ya Misenyi kwa kumfunga magoli 5-1,mechi ikichezwa uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Ushindi huo unawafanya Kumuyange FC kuandika rekodi ya kuubeba Ubingwa wa Mkoa bila kupoteza mechi yake hata moja,ikishinda zote toka hatua ya makundi na ligi ndogo na sasa inaubeba Ubingwa kwa kujikusanyia Pointi 9.

Kumuyange FC walipata ushindi kwa Goli za Ezekiel Aizaki dk 3, Dennis Msuva la dk 44, 47, na 73 na la 5 likifungwa Ibrahim Kungu dk 81 wakati  Eleven Stars likifungwa na Emanuel Sam dk 27.

Furaha ya Ubingwa ikiendelea kwa Timu ya Kumuyange FC ya Ngara.


Mashabiki wa Eleven Stars wakiwa hawaamini kinachotokea kwa Timu yao dhidi ya Timu ya Kumuyange FC ya Ngara  baada ya kumvua Ubingwa huo Timu ya Eleven Stars ya Misenyi kwa kumfunga magoli 5-1.

Timu ya Kumuyange FC ya Ngara.









Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Ngara -NDFA sambamba na Mwenyekiti wa Timu ya Kumuyange FC ya Ngara wakifurahia Ubingwa wa Soka mkoani Kagera 2017 /2018 baada ya kumvua Ubingwa huo Timu ya Eleven Stars ya Misenyi kwa kumfunga magoli 5-1 Jana January 14,Kaitaba Bukoba.


Said Mazagazaga mwenye shati la kijani akipokea Kombe na Zawadi ya Seti moja ya Jezi na Mpira mmoja baada ya kuibuka washindi wa Pili.

Mchezo wa mchana saa nane, Mazagazaga FC ya Biharamulo imeshika nafasi ya pili kwa kujiongezea point na kufikisha 4 baada ya kuifunga Vatican FC ya Muleba mabao 2-1.

Goli mbili za Huruma Shamba dk ya 2 na 34 akiipa Mazagazaga FC ushindi huo huku lile la Vatican FC likiwekwa kambani na Nelson Richard dk ya 53 kipindi cha pili kwa njia ya penati.

Eleven Stars imemaliza kwa kushika nafasi ya 3 na Pointi 4 huku ikifungwa mabao mengi tofauti na Mazagazaga FC na Vatican FC ya Muleba ikiburuza bila Pointi baada ya kufungwa mechi zote 3.

Kumuyange FC ilikabidhiwa Kombe la Ubingwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi-CCM Manispaa ya Bukoba, Bw. Muganyizi Zachwa sambamba na Jezi seti moja na Mipira miwili.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad