Ajali ya Hiace na Malori 3 kugongana Biharamulo yaua 11 Mpaka sasa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 15, 2018

Ajali ya Hiace na Malori 3 kugongana Biharamulo yaua 11 Mpaka sasa.

Watu wawili wamefariki wakati wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo na kufikisha idadi ya watu 11 kufuatia ajali ya gari iliyotokea jana katika kijiji cha Mugera kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera,wakati wakisafiri kutoka wilaya ya Kibondo mkoni Kigoma kuelekea wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mganga Mkuu wa Hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo,Mkoani Kagera, Dr. Gresimus Sebuyoya amesema kuwa majeruhi waliofikishwa hospitalini walikuwa saba lakini wawili walifariki muda mfupi kutokana na kuvuja damu nyingi.

Aidha amesema kuwa watu tisa walifariki papo hapo mara baada ya ajali kutokea majira ya saa kumi za jioni na majeruhi watano waliobakia wanaendelea kupatiwa matibabu.

Dr Sebuyoya amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Juma Samo (25) Joseph Otieno (30), Oscar Leonard Sebastian (27), Baseke Mashinga Nyabashiki (31), Mahalulo Charles (25) na majeruhi wa sita hajafahamika kwa kuwa hajajitambua na kwamba maiti waliofia eneo la tukio ni Tisa na wawili wamefariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Mugera Bw Mapunda Kayuki amesema ajali hiyo imetokea jana January 14, 2018 majira ya Saa 11 jioni ambapo gari la Abiria aina ya Hiace lilitaka kukwepana na roli kwenye barabara ya Nyakanazi-Kahama kwenye kijiji hicho na kugongana ambapo dereva wa Hiace na Konda wake ni miongoni mwa waliofariki.

Hiace hiyo yenye namba za usajili T 542 DKE ilikuwa ikitokea Kibondo kwenda Kahama ambapo maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo ni T 860 CGS, T 103 DUJ na T 147 DUJ ambapo magari yako chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad