Samaki Wachanga wa Tani Sita zanaswa Sengerema. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 19, 2018

Samaki Wachanga wa Tani Sita zanaswa Sengerema.

Tani sita za shehena ya samaki wachanga na wazazi aina ya Sangara yenye thamani ya Sh 24 milioni imekamatwa juzi katika Kijiji cha Kawekamo, Kata ya Nyampande wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Ilidaiwa kuwa samaki hao waliokutwa wameanikwa kijijini hapo walikuwa kwenye harakati za kupelekwa nje ya nchi kimagendo.

Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema, Alen Augustine alisema kazi ya kukamata shehena hiyo ilifanikiwa baada ya vyombo vya dola kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu mipango ya kusafirisha samaki hao kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Katika zoezi hilo, pia tumefanikiwa kukamata nyavu 012 za kuvuli samaki zenye matundu ya nchi 4.5 na sita zenye thamani ya Sh 22.9 milioni,” alisema Augustine.



Kaimu Ofisa Uvuvi, Halmashauri ya Sengerema, Benerdictor Magaonda aliahidi kuwa ofisi yake itaendelea kuwasaka na kuwatia mbaroni wote wanaojihusisha na uvuvi haramu na biashara ya samaki bila kuzingatia sheria.

Ofisa Mtendaji Kata ya Nyamapande, Wiliam Donart aliwaomba wananchi kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya uvuvi na biashara haramu ya Samaki.

Alisema mapambano hayo yatasaidia kulinda rasilimali hiyo kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.     

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad