Wagombea 27
wa ubunge na udiwani wameteuliwa kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mdogo
utakaofanyika Februari 17, mwaka huu katika majimbo mawili ya ubunge na kata
nne.
Katika
uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, mgombea udiwani kupitita CCM
katika kata ya Kimagai iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani
Dodoma, amepita bila kupingwa.
Mbali na
uteuzi huo, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika kata sita za Tanzania Bara
wanatarajia kuteua wagombea wa udiwani wa kata hizo siku ya Jumatano ya tarehe
24 Januari, 2018 kukamilisha kata 10 zilizopangwa kushiriki Uchaguzi Mdogo wa
Februari 17, 2018.
Akizungumzi
uteuzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
Hamis Mkunga amesema mgombea huyo wa CCMa amepita bila kupingwa baada ya mgombea
wa CHADEMA kushindwa kurejesha fomu za uteuzi.
Amesema
katika uteuzi wa wagombea Jimbo la Kinondoni, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo
hilo amewateua wagombea 12 ambao ni ambao ni Godfrey Maliza kutoka chama
cha TLP, Johnson Mwangosya (SAU) na Mwajuma Milambo kutoka UMD.
Mkunga
amewataja wagombea wengine walioteuliwa kuwa ni John January Mboya
(Demokrasia Makini), Maulidi Mtulia (CCM), na Mary Mpangala wa DP.
Wengine ni
Salim Mwalimu (CHADEMA), Rajabu Salum (CUF), Mohamed Majaliwa (NRA),
George Christian (CCK), Ally Omari Abdallah (ADA THADEA) na Ashiri
Kiwendu wa AFP
Kuhusu
uteuzi wa wagombea ubunge katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro, Mkunga
amewataja wagombea wanne walioteuliwa kuwa ni Dk Godwin Mollel (CCM) Mdoe
Azania Yambazi (SAU), Tumsifuheri Mwanry (CUF) naElvis Christopher MosiwaCHADEMA.
Katika kata
tatu zilizobaki, Mkunga amevitaja vyama vya siasa vilivyopitisha wagombea ambao
waliteuliwa katika kata ya Isamilo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana
mkoa wa Mwanza kuwa ni Chama cha CUF, DP, UDP, CCM, na CHADEMA.
Amevikumbusha
vyama na wagombea kuheshimu maadili ya uchaguzi katika kipindi hiki cha kampeni
kwani vyama vyote vimekubaliana kuheshimu maadili hayo na kuwaomba wananchi
wajitokeze kwa wingisiku ya kupiga tarehe 17 Februari mwaka 2018.
Na Hussein
Makame-NEC
No comments:
Post a Comment