Picha- Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigina –Ngara wafurahi kwa Kucheza Michezo ya Jambo Bukoba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 25, 2018

Picha- Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigina –Ngara wafurahi kwa Kucheza Michezo ya Jambo Bukoba.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigina,wilayani Ngara mkoani Kagera  wakicheza mchezo wa Tuvutane Kiuno ikiwa ni moja ya michezo inayoandaliwa na Shirika la Jambo Bukoba la Kagera wakati wa muda wa Michezo Shuleni hapo ambapo waliongozwa na Mwalimu wao wa Michezo –Mwl.Mwandu Joseph Kusigwa  kufundishwa na kucheza michezo hiyo mbalimbali inayoandaliwa na Shirika la  Jambo Bukoba la Mkoani Kagera, Jana January 24, 2018  katika viwanja vya Shule hiyo.

Jambo Bukoba ni Shirika lisilokuwa la Serikali linalofanya kazi mkoani Kagera kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa. 

 Jambo Bukoba ilianzishwa Mkoani Kagera kwa kusaidia watoto hasa Wanafunzi wa Shule za Msingi kuanzia miaka 5 hadi 19 kujenga Afya zao Kimichezo ili kujikinga na Maabukizi ya UKIMWI, kuweka haki sawa katika Elimu kupitia michezo kwa Wasichana na Wavulana. 

Tangu kuanzishwa kwake mkoani Kagera limekuwa likiwafunza watoto katika shule za msingi kila wilaya michezo midogo midogo ya kujenga ushirikiano wa pamoja hasa watoto wa kike kujiamini na kushirikiana zaidi na wenzao wa kiume.
Wanafunzi hao wa Shule ya Msingi Kigina,walicheza pamoja na kufundishwa michezo ya Pasi Kumi,Tushikane Mabega,Tuvutane  Kiuno, Kiti Kisichokuwa na Mwisho na Mpira Huru.



Mwalimu wao wa Michezo –Mwl.Mwandu Joseph Kusigwa  akiwafundisha Wanafunzi wake wa Shule ya Msingi Kigina,kucheza mchezo wa Kiti Kisichokuwa na Mwisho.


Wanafunzi hao wa Shule ya Msingi Kigina,walicheza mchezo wa  Mpira Huru.


 Tangu kuanzishwa kwake mkoani Kagera Jambo Bukoba limekuwa likiwafunza watoto katika shule za msingi kila wilaya michezo midogo midogo ya kujenga ushirikiano wa pamoja hasa watoto wa kike kujiamini na kushirikiana zaidi na wenzao wa kiume.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad