Askofu Niwemugizi na Waraka Mzito. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 14, 2017

Askofu Niwemugizi na Waraka Mzito.

Baada ya kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusu uhalali wa uraia wake Askofu wa Jimbo la Ngara - Rulenge, Severine Niwemugizi ameeleza kwamba amezungumza na Rais John Magufuli.

Jana, askofu huyo alikaririwa akisema amehojiwa mara mbili na Uhamiaji katika kile kinachoelezwa ni utata wa uraia wake huku akieleza kuwa amezaliwa wilayani Biharamulo mkoani Kagera.

Alipoulizwa kama mazungumzo hayo  na Rais Magufuli ni baada ya taarifa za kuhojiwa na Uhamiaji, Askofu Niwemugizi alijibu huku akianza kwa kucheka, “Hahahahaha!! Ni kweli Rais kataka kujua hasa kuna nini, yeye amesema atalifuatilia na kukiwa na... nitamfahamisha.”

Askofu huyo ambaye Septemba mwaka huu aliibua mjadala wa Katiba Mpya na kusema kuwa yuko tayari kuitwa mchochezi endapo kundi la watetezi wa haki za binadamu watachukuliwa kama wachochezi alisema kuhojiwa huko hakutamrudisha nyuma katika misimamo yake, “Siwezi kurudi nyuma, nimetumwa na Kristo, Nabii anaweza kupendwa au kuchukiwa na mimi siwezi kunyamaza.”

Askofu Niwemugizi aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) alisema, “Mimi nazungumza lakini kuna Watanzania wengine wanazungumza sana. Lakini mimi kuhojiwa mara mbili hakutaninyamazisha.”

Ujumbe aliouweka Facebook, unasema, “Nasali Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki, uniokoe na mtu wa hila asiye haki. Kwa kuwa wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa?

Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea? ...Nafsi yangu, kwa nini kuinama, na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; kwa maana nitakuja kumsifu, aliye afya ya uso wangu na Mungu wangu” (Zab 43:1-2,5). Asante Rais wangu JPM kwa faraja uliyonipa.”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad