Dimba la Chamazi kutumika kwa Simba SC na Yanga SC mechi zao Zijazo VPL. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 20, 2017

Dimba la Chamazi kutumika kwa Simba SC na Yanga SC mechi zao Zijazo VPL.


Simba ilipocheza na Azam FC kwa mara ya kwanza katika dimba la Chamazi, Dar Es Salaam.

Mechi ya ligi kuu Tanzania bara kati ya Yanga SC vs Tanzania Prisons, na mechi kati ya Simba SC vs Lipuli FC zilizopangwa kuchezwa tarehe 25 na 26 mwezi huu, sasa zitapigwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi badala ya Uwanja wa Uhuru kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Taarifa iliyotolewa na bodi ya ligi imesema kuwa sababu ya kuhamisha mechi hizo ni mmiliki wa Uwanja wa Uhuru (Serikali) kuutumia uwanja huo kwa shughuli nyingine za kijamii kuanzia tarehe 24 hadi 27 mwezi huu.

Mechi zote za raundi ya 11 zitakazopigwa wikiendi ijayo ziko kama ifuatavyo.
Ijumaa ya tarehe 24, Novemba utapigwa mchezo mmoja ambapo Ndanda FC itakuwa nyumbani kuwakaribisha Njombe Mji.

Jumamosi ya tarehe 25, Novemba, kutakuwa na mechi tano kama ifuatavyo:-

Yanga SC vs Prisons

Singida United vs Mbeya City

Mbao FC vs Mwadui

Kagera Sugar vs Stand United

Ruvu Shooting vs Majimaji FC

Jumapili ya Novemba 26 ni mechi moja itakayowakutanisha vinara wa ligi hiyo, Simba SC watakaowakaribisha Lipuli FC na Jumatatu ya Novemba 27, Azam FC watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar, mchezo utakaopigwa Chamazi Dar es Salaam saa 1:00 usiku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad