UEFA Champions League 2017/2018 - Cristiano Ronaldo na Rekodi,Real Madrid ikiishinda Borussia Dortmund. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 27, 2017

UEFA Champions League 2017/2018 - Cristiano Ronaldo na Rekodi,Real Madrid ikiishinda Borussia Dortmund.

Jana September 26,2017 Usiku Michezo nane ya UEFA Champions League  2017/2018 ilichezwa barani Ulaya na moja kati ya mchezo wa kuvutia ulikuwa ni mchezo kati ya Borussia Dortmund dhidi ya Real Madrid ya Hispania ambao walikuwa ugenini.

Mchezaji Cristiano Ronaldo (kulia) alishangilia akiwa na wenzake  Gareth Bale baada ya kufunga bao la pili la Real Madrid dakika ya 49 katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Borussia Dortmund kwenye mchezo wa Kundi H  wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park mjini Dortmund.

 Bale aliyetoa pasi la bao la pili, ndiye aliyefunga bao la kwanza dakika ya 18, wakati Ronaldo alifunga na la tatu pia dakika ya 79 na Pierre-Emerick Aubameyang akawafungia wenyeji la kufutia machozi dakika ya 54.
Kufunga magoli mawili kwa Cristiano Ronaldo kunamfanya kuzifunga timu za Ujerumani kwa mara ya 25 akicheza dhidi yao kwa mechi 21, hata hivyo usiku huo umemfanya Ronaldo kufikisha jumla ya game 400 akiichezea Real Madrid akiwa kafunga jumla ya magoli 411, assist 111 na amefunga jumla ya hat-trick ya 42.

MSIMAMO WA KUNDI H.
MATOKEO YA MECHI ZINGINE JANA. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad