“Ninafahamu
baadhi ya wafungwa hawa wapo wengi wanaosubiri kunyongwa hadi kufa, na marais
waliopita walikwepa jukumu la kusaini sheria hii, na mimi nakuomba Jaji Mkuu
usiniletee kwa sababu nafahamu ugumu wake,” alisema Rais Magufuli.
Tamko hilo
la Rais Magufuli limeungwa mkono na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
ambapo wamesema kwamba sheria ya kifo inakiuka haki ya kuishi na inatweza utu
wa binadamu.
|
Kwa upande
mwingine Rais Magufuli amewapongeza majaji wote waliopo kazini na wastaafu na
kusema kwamba wanafanya/walifanya kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi.
Kwa upande
wake Jaji Mkuu, miongoni mwa mambo mengi aliyoyazungumza ni pamoja na kutolea
ufafanuzi taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa na watu kuwa kuna muingiliano
katika mihimili ya serikali.
Akitolea
ufafanuzi hilo alisema si kweli kwamba kuna muingiliano unaodaiwa, bali kuna
wakati muhimili hiyo lazima ikae pamoja kuwatumikia wananchi lakini kila mmoja
una majukumu yake ya kutekeleza.
|
No comments:
Post a Comment