Taharuki
Bungeni (Picha na maktaba).
WABUNGE wa
CUF wameonekana kuvurugana Bungeni Mjini Dodoma Jana Jumatatu, Septemba 11,2017
kutokana na mgogoro unaoendelea katika chama hicho baada ya wabunge wanaomuunga
mkono Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya uchaguzi na kumchagua Mbunge wa
Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma kuwa mwenyekiti wao Bungeni.
Naibu Spika
wa Bunge, Dk Tulia Ackson alitangaza kuwa Spika, Job Ndugai amepokea barua
kutoka kwa Katibu wa CUF, Magdalena Sakaya kuhusu safu hiyo ya uongozi.
Baada ya
tangazo hilo, Mbunge wa Malindi, Ally Salehe aliomba mwongozo wa Spika
akitaka kujua ni nani anaamua kuhusu
uongozi wa Wabunge Bungeni kwa sababu wao wameshafanya uchaguzi na kumchagua
Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea kuwa Mwenyekiti wao baada ya kufukuzwa kwa
Wabunge wanane.
Pia, amehoji inawezekanaje kuwa na viongozi wawili bila wa
kwanza kufutwa?
Akijibu
mwongozo huo, Dk Tulia amesema Spika amepokea taarifa ya viongozi hao lakini
hajapokea taarifa ya uchaguzi wa upande wa akina Ally Salehe ambao unamuunga
mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. Amesema watakapopeleka
taarifa yao ndipo Spika ataamua.
|
No comments:
Post a Comment