Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (aliyeshika mkasi) akikata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners
handbook), Toleo la Pili, kilichoandikwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi
(ISS), tukio hilo limefanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini,
Kampasi ya Dodoma.
|
Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (katikati), akionesha kitabu
cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, baada ya kukizindua rasmi katika Chuo cha
Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma.
Wa pili kushoto ni Kaimu Balozi wa Uholanzi
hapa nchini, Bi. Lianne Houben, na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la
Uongozi la Chuo hicho Prof. Razack Lokina.
|
Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi Kaimu Mkuu wa
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, nakala ya Kitabu
cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya
kukizindua rasmi mkoani Dodoma.
|
Kaimu Balozi
wa Uholanzi hapa Nchini, Bi. Lianne Hauben (kushoto), akifurahi wakati
akikabidhiwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb),
nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la
Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.
|
Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi Mwenyekiti wa
Baraza la Uongozi la Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Razack Lokina,
nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa wanamipango (Planners Handbook), Toleo la
Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.
|
Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi
wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Kanda ya Ziwa, Dkt.
Benedict Kilobe, nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners
Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.
Benny
Mwaipaja, Dodoma
Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezindua Kitabu cha Mwongozo kwa
Wanamipango Tanzania, kilichoandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini
kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), na
kuwataka wataalamu wa mipango hapa nchini kuandaa mipango yenye tija
itakayoiwezesha jamii kuondokana na umasikini.
Dkt. Kijaji
ameeleza kuwa nafasi ya wataalamu wa mipango katika kukuza uchumi wa nchi ni
kubwa na kwamba kinachotakiwa ni kuandaa mipango shirikishi itakayochangia
kuimarisha maisha ya wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi.
“Ni
matumaini yangu makubwa kwamba kuzinduliwa kwa kitabu hiki cha mwongozo kwa
wanamipango, kutakuwa chachu ya wataalamu wetu kuangalia namna ya kupeleka
maendeleo vijijini na sehemu nyingine duniani kwa kutoa wataalamu waliobobea ili
kuharakisha maendeleo ya nchi” alisistiza Dkt. Kijaji
Ameeleza
kuwa maudhui ya kitabu hicho yapelekwe hadi ngazi za chini kupitia Serikali za
Mitaa ili watu wengi waweze kukisoma na kuelekezwa namna bora ya kupanga
mipango yao ya maendeleo.
Kwa upande
wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijini, Prof. Hozen Mayaya,
amesema kitabu hicho kimelenga kuwaongezea ujuzi wataalamu wa mipango kwa
kuzingatia vitendo zaidi badala ya nadharia.
“Kitabu cha
Mwongozo kwa wanamipango kitakuwa rejea ya nadharia nyingi na njia ambazo
wataalamu wanapaswa kuzijua, namna ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na
kuifanya mipango iweze kutekelezeka kama ilivyokusudiwa” alisema Prof. Mayaya.
Nae Kaimu
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Bi. Lianne Houben, ambaye kwa namna moja au
nyingine nchi yake imefadhili uandishi na uchapaji wa mwongozo huo, toleo la
pili, amesema nchi yake inajivunia uhusiano imara uliodumu kwa miongo kadhaa na
Tanzania.
Alisema kuwa
mtazamo wa ushirikiano wake na Tanzania kuanzia mwaka huu ni kujikita zaidi
katika uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na kwamba uwekezaji wao mkubwa
utalenga pia kuboresha kilimo na usalama wa chakula.
“Uholanzi ni
nchi ya pili katika kufanya biashara na Tanzania ikitanguliwa na Marekani
ambapo mwaka 2016, Uholanzi, imenunua bidhaa zenye thamani ya Euro bilioni 85”
aliongeza Bi. Houben
Aidha,
alieleza kuwa nchi yake imetoa mchango mkubwa katika kuendeleza rasilimali watu
ambapo hadi sasa wanafunzi na wataalaamu katika fani mbalimbali wapatao 5,000,
wamepata mafunzo kutoka katika vyuo mbalimbali nchini Uholanzi.
|
No comments:
Post a Comment