|
Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma Jana September
16,2017 aliinusuru timu yake, Yanga SC
kupoteza mechi mbele ya Maji Maji baada ya kuifungia bao la kusawazisha kipindi
cha pili, timu hizo zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ngoma
alifunga bao la kusawazisha dakika ya 79 kwa kichwa akimalizia krosi ya
Mzambia, Obrey Chirwa huku Maji Maji FC kutangulia kwa bao la Peter Mapunda dakika ya 54 akimalizia
pasi ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Jerson John Tegete kumtungua kipa Mcameroon Youthe Rostand.
Matokeo ya Mechi nyingine za Jana
nimekuwekea hapo Juu na hapa chini ni Ratiba ya leo September 17,2017 na Msimamo ulivyo baada
ya mechi za Jana.
|
No comments:
Post a Comment