EPL 2017/2018- Ubabe mwingi Chelsea na Arsenal waleta kadi na Sare. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 17, 2017

EPL 2017/2018- Ubabe mwingi Chelsea na Arsenal waleta kadi na Sare.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Chelsea wamelazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa vuta nikuvute uliochezwa leo September 17,2017 kwenye uwanja wa Stamford Bridge. 

Tukio kubwa zaidi kwenye mchezo huo, ni kupewa kadi nyekundu kwa beki wa Chelsea David Luis kunako dakika ya 86 baada ya kumchezea rafu beki tatu wa Arsenal Sead Kolasinac.

Baadhi ya wachambuzi wakiwemo Alan Shearer na Peter Schmeichel wamepata kigugumizi juu ya kadi hiyo nyekundu huku wengi wao wakiamini kadi njano ingekuwa uamuzi sahihi. 


Mchezo huo uliojaa ufundi wa kila namna, pia ulitawaliwa na ubabe mwingi na kumpelekea mwamuzi Michael Oliver kutoka kadi za njano mbili kwa Chelsea na tatu kwa Arsenal.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad