VPL 2017/2018 - Simba SC na Mbeya City wawatafuna Mwadui FC na Njombe Mji FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 17, 2017

VPL 2017/2018 - Simba SC na Mbeya City wawatafuna Mwadui FC na Njombe Mji FC.

Emmanuel Okwi katikati pichani akishangilia na wachezaji wenzake wa Simba SC baada ya kufunga mabao mawili leo September 17,2017 dhidi ya Mwadui FC.

Mabao yote ya Simba leo yalikuwa mazuri na yenye kudhihirisha uwezo binafsi wa wachezaji kufunga na kwa ujumla, Wekundu wa Msimbazi walikuwa katika mechi nyepesi mno jioni hii.

Simba SC imewapa burudani ya nafsi mashabiki wake leo September 17,2017 baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Simba SC, John Bocco.

Nyota wa mchezo wa leo kwa mara nyingine amekuwa mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyefunga mabao mawili na kufikisha mabao matano katika mechi mbili tu za Ligi Kuu alizocheza msimu huu, kufuatia kufunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa kwanza.
Hapa chini Matokeo ya Mechi za Jana September 16,2017.

Msimamo wa VPL 2017/2018 Ulivyo sasa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad