Taswira Picha Nyumba zaidi ya 90 zilizovamia Hifadhi zikichomwa Moto wilayani Biharamulo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 12, 2017

Taswira Picha Nyumba zaidi ya 90 zilizovamia Hifadhi zikichomwa Moto wilayani Biharamulo.

August 22, 2017 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu alifanya ziara katika Wilaya ya Biharamulo ambako alisisitiza juu ya kutekelezwa maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo kuwa watu wote wanaoishi katika maeneo ya hifadhi ya misitu kuondoka kabla ya September 9 mwaka huu.

Wakitekeleza maagizo hayo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo ya Biharamulo, Bi. Saada Malunde, wameteketeza kwa moto nyumba zaidi ya 90 katika hifadhi ya msitu wa Nyantakara eneo maarufu kama “Mombasa Raha” ikiwa ni pamoja na kukamata ng’ombe saba na kuteketeza mashamba yaliyoanzishwa ndani ya hifadhi hiyo.
Mkuu wa wilaya hiyo ya Biharamulo, Bi. Saada Malunde.

Meneja Misitu ya Hifadhi wilayani Biharamulo Bw.Emmanuel Komba amesema kuwa vijiji ambavyo vinaanzishwa katika maeneo ya mistu bila kufuata taratibu ni kosa kisheria na inaathiri sana uhifadhi  na ni sehemu moja wapo ya watu wanaohujumu uchumi wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad