Aidha,
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu 2017 ,Bw.Amour Hamad Amour
akizindua mabweni mawili ya wavulana katika Shule ya Sekondari Bugene
yaliyojengwa kwa gharama ya shilingi 152 milioni fedha za Serikali Kuu,
aliwaasa wanafunzi wa shule hiyo yenye
kidato cha tano na sita kusoma kwa bidii ili wayafikie malengo yao na malengo
ya wazazi wao pia.
Bw. Amour
alisema kuwa ili wanafunzi hao waweze kufaulu vizuri ni lazima wawe na nidhamu
ya hali ya juu hasa kwa walimu wao wanaowafundisha pia kujiheshimu wao wenyewe
na kuzingatia masomo na maadili wanayofunzwa shuleni hapo.
Pia Bw.
Amour aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya
kuwafundisha wanafunzi kwa umakini mkubwa na kupelekea kupata matokeo mazuri ya
kidato cha sita kwa mwaka 2017.
Pia aliwasihi kuhakikisha wanazingatia maadili
ya taaluma yao wanapokuwa wanawafundisha wanafunzi hao.
|
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2017 alitoa angalizo kwa
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bugene kuwa ni lazima kuangalia nidhamu za
walimu wake na kuchukua hatua mapema kwa mwalimu atakayekwenda kinyume na
maadili ya kazi yake kabla yeye Mkuu wa Shule hajachukuliwa hatua na Serikali
ya awamu ya tano.
|
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Karagwe Bw. Godfrey Mheruka akimshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru 2017 alisema kuwa uongozi wa Wilaya uliamua kupeleka Mwenge wa Uhuru
katika Shule ya Sekondari Bugene baada ya shule hiyo kufanya vizuri katika
matokeo yake ya kidato cha sita 2017 ambapo walifaulu kwa ( Daraja la I = 13,
Daraja la II =41, Daraja la III =22 na Daraja IV =2 aidha hakuna mwanafunzi
aliyepata sifuri)
Mwenge wa
Uhuru tayari unaendelea na mbio zake Mkoani Kagera katika Halmashauri ya
Wilaya ya Kyerwa leo tarehe 4 Agosti, 2017.
|
No comments:
Post a Comment