Watumishi 450 washinda Rufaa Vyeti Feki Tanzania, Kurudishwa Kazini. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 14, 2017

Watumishi 450 washinda Rufaa Vyeti Feki Tanzania, Kurudishwa Kazini.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora imetangaza kuwa watumishi wa umma 450 wameshinda rufaa, kati ya waombaji 1,050 ambao waliwasilisha rufaa zao katika mamlaka husika baada ya kutajwa katika orodha ya wenye vyeti feki.

 Akizungumza na wanahabari jana July 13,2017 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora, Dk Laurian Ndumbaro alisema serikali iliendesha uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu ambako watumishi wa umma 9,932 walikutwa na vyeti feki.

Baada ya kutangazwa kwa orodha hiyo ya watumishi wenye vyeti feki, watumishi 1,050 walikata rufaa na watumishi 450 pekee walishinda rufaa hizo huku watumishi 8,800 wakiridhika na matokeo hayo,” alisema Dkt Ndumbaro

Kuna baadhi ya walitumia majina mawili alipokuwa kidato cha nne baadae alilazimika kutumia matatu na kubadilisha mkanganyiko hivyo tumejiridhisha na wanarudishwa katika utumishi wa umma.”

Aidha Ndumbaro aliongeza kuwa rufaa hizo zilizokubaliwa ni kwa watumishi wale waliokuwa wakitumia majina ya waume zao baada ya kuolewa, ambayo yalitofautiana na majina yaliyopo kwenye vyeti na baada ya uhakiki walionekana kama ni vyeti feki.

Katika hatua nyingine, Dk Ndumbaro alizungumzia suala la ajira mpya, ambapo alisema serikali imeanza kutoa vibali vya ajira mpya kuanzia mwezi ujao, watatangaza nafasi hizo na Watanzania wenye sifa watajaza nafasi hizo 10,184 na nyingi zikiwa kwenye sekta ya afya na elimu.

Post Bottom Ad