Picha-Simba akimnyonyesha Mtoto wa Chui, Nchini Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 14, 2017

Picha-Simba akimnyonyesha Mtoto wa Chui, Nchini Tanzania.


Mwana wa chui hawezi kubadili madoa doa katika ngozi yake lakini simba huyo hajali hilo.

Picha hizi ni za kwanza kuchukuliwa simba akimnyonyesha mwana wa chui kutoka jamii nyengine ya wanayama, kisa kisicho cha kawaida.

Wawili hao walionekana na Joop Van Der Linde mgeni katika katika eneo la Ndutu Safari Lodge nchini Tanzania katika eneo la uhifadhi la wanyma pori la Ngorongoro.
Simba wengi wa kike huwauwa watoto wa chui wanapokutana nao, na huwaona kama wapinzani katika mapambano ya kutafuta chakula.

Simba huyo alikuwa kilomita moja kutoka kwa nyumba yao ambapo kuna maficho ya watoto wake alipokutana na chui huyo mdogo.

Alimchukua mwana huyo na kumlea kama wake na humlindi dhidi ya shambulio lolote.
Daktari Luke Hunter , ambaye ni rais muhifadhi mkuu wa Panthera ,shirika kuu la ufugaji wa wanyama aina ya paka aliambia BBC kwamba kisa hicho ni cha kipekee.
Simba Nasikitok akimnyonyesha mwana huyo wa chui katika Ngorongoro.

Eneo hilo ni la Serengeti. Simba huyo amepewa jina Nosikitok na ana umri wa miaka mitano.

Simba huyo amewekewa mfumo wa GPS katika shingo yake ili kutambua anakokwenda na ana watoto watatu waliozaliwa kati ya mwezi Juni 27-28.
Chui mtoto anayeishi na Simba


Post Bottom Ad