Changamoto la Maji Kasange latua mikononi mwa Mbunge wa Jimbo la Ngara Alex Gashaza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 30, 2017

Changamoto la Maji Kasange latua mikononi mwa Mbunge wa Jimbo la Ngara Alex Gashaza.

Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw.ALex Rafael Gashaza mwenye kofia nyekundu akiwasikiliza wananchi juu ya kero ya maji katika kisima cha maji kijiji cha Kasange wilayani Ngara mkoani Kagera.

Wananchi wa Kijiji cha Kasange,Kata ya Kirushya wilayani Ngara mkoani Kagera  wana kabiliwa na changamoto ya uhaba wa  Maji kwa kipindi kirefu hali ambayo hupelekea wananchi kushindwa kufanya shughuli za maendeleo kwa kukaa kisimani kwa muda mrefu wakisubiria huduma ya maji kutoka na foleni ya watu ambayo husababishwa na maji kutoka kidogo kidogo huku idadi ya watu ikiwa kubwa.

Wakizungumza na Mwanawamakonda blog  kisimani hapo wamesema kuwa wanapata adha kubwa ya maji licha ya kuwa na kisima cha maji lakini kisima hicho hakitoshelezi mahitaji ya wananchi.

Katika kisima hulazimika kuchota watu wenye nguvu huku watoto walio agizwa na wazazi wao wakiishia kuangalia kwana hawa nguvu za kusukumana ilikuweza kuchota maji hayo.
Niwaombe wakazi wa kijiji cha kasange kata ya kirushya kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu  mimi kwa kushirikiana naserikali tunatafuta namna ya kuweza kuwa saidia wananchi hawa natambua kuwa tatizo la maji ni tatizo la kitaifa lakini niwaombe kuvuta subira nafanya kila liwezekanalo kupata wafadhili ili kuweza kujenga tenki la maji kubwa pamoja na pampu kwaajili ya kusuma maji kutoka kwenye kisima hiki kujaza tenki ambalo litasaidia kusambaza maji ndani ya kijiji hicho”alisema Gashaza.

Kisima hicho ambacho uhudumia watu wengi ikiwemo raia kutoka nchi jirani ya Burundi ambao ni majirani kutokana na  kijiji  hicho kupakana na nchi ya Burundi.

Wananchi walipaza kilio chao kwa Mbunge , Bw. Alex Rafael Gashaza ili kuwasaidia kutatua changamoto ya maji katika kijiji chao ili kuondokana na usumbufu wa maji wanao upata.

Hata hivyo Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw. Gashaza amesema kuwa hivisasa yupo kwenye mchato wa kutafuta wafadhili ili kusaidia kujudi zake za kujenga Visima maeneo yaliyo na shida ya maji ili kutosheleza mahitaji ya wananchi.

Post Bottom Ad