Picha-Wafugaji Kanda ya Ziwa waenda Kumuona Waziri Mkuu baada ya Waziri Magembe kuwakacha Biharamulo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 01, 2017

Picha-Wafugaji Kanda ya Ziwa waenda Kumuona Waziri Mkuu baada ya Waziri Magembe kuwakacha Biharamulo.

Baadhi ya Wafugaji kutoka Kanda ya Ziwa.

Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa kimeunda kamati ndogo ya wafugaji 20 itakayokwenda kuonana na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Magembe kushindwa kuonana nao May 29,2017 kama walivyo ahidiwa.

Akiongea na katika kikao cha wafugaji wa kanda ya ziwa kilichofanyika May 29,2017  katika ukumbi wa Rest mjini Biharamulo,mkoani Kagera,Mwenyekiti wa chama hicho Bw Juvenary Mlashani amesema kuwa kitendo cha Waziri  Magembe kushindwa kuonana na wafugaji ambao walikua tayari wamekwisha kubaliana pamoja na Waziri Mkuu na Wabunge wa Mikoa ya Kagera na Geita

Bw Juvenary amesema kamati hiyo imeondoka kwenda kuonana na Waziri Mkuu mjini Dodoma wakiambatana na Wabunge wao, kwa lengo la kumueleza malalamiko ya kukamatwa na kuuzwa kwa mifugo yao.

Kikao cha Ndani kilifanyika na Waziri Magembe.


Awali Waziri wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Magembe ( Aliyesimama Pichani ) ameipongeza Idara ya Wanyamapoli mkoa wa Kagera kwa kufanikisha operation ya kuondoa mifugo iliyokuwa ndani ya mapori ya akiba ya hifadhi ya Biharamulo, Kimisi na Burigi na kwamba Serikali haitaruhusu tena mifugo hiyo kuingia ndani ya hifadhi

Pro. Magembe amesema kuwa operation za mara kwa mara zitakuwa zinafanyika katika mapori hayo ya hifadhi ikiwemo kurusha ndege zenye rubani na zile zisizo na rubani ili kuhakikisha mifugo yote inaondolewa lakini pia mifugo hiyo hairudishwi katika mapori hayo kama walivyozoea kufanya siku za nyuma.
 Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mhe.Oscar Mukasa akiwawawakilisha Wabunge wenzake wa Mikoa ya Kagera na Geita amesema katika kikao na Waziri Mkuu walikubaliana Waziri wa Maliasili akutane na kuzungumza na Wafugaji na kuwataka Wafugaji kuwa watulivu wakati Wabunge wao wakiendelea kuwasiliana na Serikali.
Picha ya Risiti wanazopewa Wanunuzi wa Mifugo.

Picha ya Risiti wanazopewa Wanunuzi wa Mifugo.

Picha ya Risiti wanazopewa Wanunuzi wa Mifugo.

Post Bottom Ad