Bunge la Tanzania Lapitisha Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango Shilingi Trilioni 11.752. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 01, 2017

Bunge la Tanzania Lapitisha Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango Shilingi Trilioni 11.752.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali za Wabunge wakati wakijadili Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma, ambapo Bunge hilo limepitisha Bajeti ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihitimisha mjadala wa Bajeti ya Wizara yake ambapo Bunge limepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya Wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni nje ya Ukumi wa Bunge mara baada ya Wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad