VIDEO/PICHA- Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Uzinduzi Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato Kielektroniki. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Friday, June 02, 2017

VIDEO/PICHA- Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Uzinduzi Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato Kielektroniki.

Rais Magufuli akizindua mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki akishuhudiwa na Rais wa SMZ, Dkt. Shein na VP Samia Suluhu wakati wa uzinduzi wake Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli hapo Jana Alhamisi, Juni 01, 2017 amezindua rasmi Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa njia ya Kielektroniki.
Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa serikali wakiwemo Rais wa Zanzibar, Dkt. Ally Mohammed Shein, Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na wengine, Rais Magufuli alianza kukagua Kituo cha Taifa cha Kutunzia Taarifa (Data Center), kilichopo TTCL Kijitonyama na kuridhishwa na mafanikio makubwa ya ubunifu huo.

Rais Magufuli, Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu na Rais wa Zanzibar, Dk. Ally Mohammed Shein walikabidhiwa iPads za kuwawezesha kuona mapato ya serikali yaliyokusanywa na mfumo huo wa kielektroniki.

HAPA CHINI-BOFYA PLAY KUISIKILIZA HATUBA YOTE YA RAIS MAGUFULI KATIKA UZINDUZI HUO.

Post Bottom Ad