Taswira Picha Basi la Adventure ,Kahama-Kigoma lilivyopata Ajali Eneo la Kifura-Kibondo ,hakuna Kifo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 17, 2017

Taswira Picha Basi la Adventure ,Kahama-Kigoma lilivyopata Ajali Eneo la Kifura-Kibondo ,hakuna Kifo.

Ajali hii imetokea Leo May 17, 2017,majira ya Mchana na kulihusisha Basi hili  lenye namba za Usajili T 757 AAZ  la kutoka Kahama kwenda Kigoma katika wilaya ya Kibondo kijiji cha kifura BARABARA kuu ya kutoka Kibondo kwenda Kasulu mkoani Kigoma ,Basi likiendeshwa na Salum Shija@Mwanashija lilikata hanger za front excel na kuacha njia kwenda porini.

SHUKRANI za pekee kwa mmiliki na Wafanyakazi wa Kampuni inayomiliki basi hilo ya Adventure kwa kuwa na matengenezo ya mara kwa Mara ya basi zake.
UTULIVU..

Uzoefu na uendeshaji salama wa kujihami wa Dereva@Mwanashija na utulivu wa abiria umefanya kusiwe na madhara zaidi kwa kuwa speed haikuwa kubwa na hakuyumba toka kuanzia tatizo  la gari.

Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa abiria wametoka wote salama na wameshapata usafiri mbadala na kuendelea na safari.


Post Bottom Ad