Taswira Wenger akishuhudia Crystal Palace ikishinda 3-0 dhidi ya Arsenal. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 11, 2017

Taswira Wenger akishuhudia Crystal Palace ikishinda 3-0 dhidi ya Arsenal.

Benchi la Arsenal baada ya Kipigo.

Timu ya Arsenal huenda wakapata ugumu wa kukaa nafasi ya 4 katika Ligi Kuu England msimu huu 2016/2017  ambazo inawapata nafasi ya kucheza Champions League, baada ya Jana usiku wa April 10 2017  kupokea kichapo cha magoli 3-0 kutoka kwa Crystal Palace katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Selhurst Park.
Magoli ya Crystal Palace yalifungwa  na Andros Townsend dakika ya 17, Yohan Cabaye dakika ya 63 na Luka Milivojevic kwa mkwaju wa penati dakika ya 68.
Katika mchezo huo ,Arsenal ilimaliza mchezo huo ikiambulia kumiliki mpira kwa asilimia 73 na Crystal Palace 27 na kipigo hicho kinaifanya Arsenal kufungwa kwa mara ya kwanza mechi nne mfululizo za Ligi kwa mara ya kwanza chini ya Arsene Wenger.

Matokeo haya yameiweka Arsenal nafasi ya 6 kwa pointi 54 sawa na Everton walio nafasi ya 7 wakiwa pointi sawa na Arsenal -54  huku Manchester United wakishika nafasi ya 5 kwa pointi 57 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 4 Man City lakini wao wamecheza Mechi 1 pungufu.


Mashabiki wengi wa Arsenal nao hawakubaki nyuma kumtaka Mzee Wenger wakimlalamikia  aondoke katika timu hiyo kutokana na kutopatia mataji kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Mechi nne ilizofungwa mfululizo za ugenini Arsenal na Chelsea 3-1, Liverpool 3-1, West Bromwich na Jana April 10, 2017 imepoteza 3-0 dhidi ya Crystal Palace lakini hicho kinakuwa ni kipigo cha kwanza toka Arsenal ipate ushindi wa kwanza wa EPL April 6 2017 dhidi ya West Ham United baada ya siku 53 bila kupata ushindi, mfululizo wa matokeo hayo kuna hatarisha nafasi ya Arsenal kucheza Champions League msimu ujao.

Post Bottom Ad