Taswira Picha Simba SC na Ushindi wa Kihistoria dhidi ya Mbao FC VPL 2016/2017. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, April 11, 2017

Taswira Picha Simba SC na Ushindi wa Kihistoria dhidi ya Mbao FC VPL 2016/2017.

Wekundu wa Msimbazi-Simba SC wamepata ushindi wa kihistoria  baada ya miaka 7 dhidi ya Mbao FC  wa bao 3-2 katika mechi ya Ligi kuu Vodacom Tanzania bara 2016/2017 iliyochezwa Jana April 10,2017 kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Hadi Mapumziko, Mbao FC waliongoza kwa magoli 2-0  yakifungwa Dakika za 21 na 36 kupitia George Sangija na Evangirist Benard.Hadi dakika ya 80 Simba ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0 matokeo ambayo kama yangebaki hivyo dakika 90 zinamalizika basi Wekundu wa Msimbazi wangekuwa kwenye nafasi finyu ya kutwaa taji la ligi kuu msimu huu.


Mbao FC wamefungwa mechi zao zote (mbili) walizokutana na Simba msimu huu. Kabla ya kuchapwa 3-2 leo April 10, 2017, walifungwa 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa October 20, 2016 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.

Magoli ya Simba SC yamefungwa dakika za lala salama ambapo goli lao la kwanza limefungwa dakika ya 82 na Frederick Blagnon.

Uzembe wa golikipa wa MbaoFC, Erick Ngwegwe ambaye aliuacha mpira udunde kisha akashindwa kuudaka kwa usahihi ulitua miguuni mwa Blagnon akafunga goli la pili dakika ya 90+1 na kufanya matokeo kuwa 2-2.

Wakati kila mmoja akiamini mchezo utamalizika kwa sare ya Mbao 2-2 Simba SC, Mzamiru Yassin akaifungia Simba SC goli la tatu dakika ya 90+7 kwa shuti kali baada ya beki wa Mbao kupiga kichwa mpira ambao ulitua kwa Mzamiru kisha kiungo huyo wa Simba SC kuachia mkwaju uliomshinda mlinda mlango wa Mbao FC.
Matokeo haya yamewaweka Simba SC kileleni mwa VPL wakiwa na Pointi 58 kwa Mechi 26 wakifuata Yanga SC wenye Pointi 56 kwa Mechi 25 huku Kagera Sugar ni wa 3 wakiwa na Pointi 46 kwa Mechi 26 na Azam FC, ambao Jana April 10, 2017 wametoka 0-0 na Mtibwa Sugar huko Morogoro, ni wa 4 wakiwa na Pointi 45 kwa Mechi 26.

Mbao FC inaendelea kubaki na pointi zake 27 ikiwa katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi, pointi nne zaidi ya Toto Africans ambayo ipo katika timu tatu zitakazoshuka daraja.

Simba SC wataendelea kubaki jijini Mwanza wakisubiri kucheza dhidi ya Toto Africans timu ambayo imekuwa mwiba kwa ‘mnyama’ hususan mechi inapochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

VPL 2016/2017: MBIO ZA UBINGWA – YANGA SC v SIMBA SC.
TAREHE
YANGA SC.
SIMBA SC

12 Aprili 
Toto Africans [Kirumba]
6 Mei
Tanzania Prisons [Taifa]
7 Mei
African Lyon [Taifa]
9 Mei
Kagera Sugar [Taifa]

13 Mei
Mbeya City [Taifa]
14 Mei
Stand United [Taifa]***
16 Mei
Toto Africans [Taifa]

20 Mei
Mwadui [Taifa]

Mbao FC [Kirumba]
***Tarehe Haijathibitishwa

Post Bottom Ad