EPL -2016/2017- Vinara Chelsea walizwa, Manchester United sare huku Liverpool wakitakata dhidi ya Everton. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Saturday, April 01, 2017

EPL -2016/2017- Vinara Chelsea walizwa, Manchester United sare huku Liverpool wakitakata dhidi ya Everton.

Vinara wa Ligi kuu soka Uingereza ,Chelsea wametandikwa mabao 2-1 wakiwa kwao Stamford Bridge walipocheza na Crystal Palace.

Katika mchezo huo wa leo April 1, 2017,Joni ,Chelsea walitangulia kufunga kupitia kwa Cesc Fabregas na Crystal Palace wakakomboa goli hilo  dakika za 9 na 11 kwa Bao za Wilfried Zaha na Christian Benteke.

Chelsea, ambao walikuwa hawajafungwa kwao Stamford Bridge katika Mechi 10 za Ligi ya EPL tangu wafungwe Septemba,2016 sasa uongozi wao wa Ligi umebaki Pointi 7 baada ya Timu ya Pili Tottenham kuichapa Ugenini 2-0 Burnley.

Bao za Spurs zilifungwa Kipindi cha Pili na Eric Dier na Son Heung-min.
Nao Mabingwa Watetezi Leicester City sasa wameanza kujihakikishia usalama wao kubaki EPL baada kupata  ushindi wao wa 4 mfululizo kwenye EPL, ikiwa ni Rekodi kwa Meneja wao Craig Shakespeare ya kuwa Meneja wa kwanza Mwingereza kushinda Mechi zake 4 kwanza za EPL.

Leo Leicester wakiwa kwao King Power Stadium waliifunga Stoke City 2-0 kwa Bao za Wilfred Ndidi na Jamie Vardy.

Huko Old Trafford, Man United walitoka 0-0 na West Bromwich Albion.
Nao Liverpool iliongezea matumaini ya kuendelea kusalia katika kundi la timu nne bora baada ya kuwatandika Everton mabao 3-1 katika Champions League.

Sadio Mane aliwapa Liverpool bao la mapema kufuatia ushirikiano mzuri na Roberto Firmino.

Bao la pili lilifungwa na Philipe Coutinho baada ya kuwabwaga wachezaji wawili wa Everton.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

Jumapili Aprili 02,2017.

1530 Swansea City v Middlesbrough     
          
1800 Arsenal v Manchester City      
     
MSIMAMO WA EPL -2016/2017.

Post Bottom Ad