Walimu 7,460 Sekondari kuhamia Msingi Nchini Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 31, 2017

Walimu 7,460 Sekondari kuhamia Msingi Nchini Tanzania.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Elimu, Bernard Makali.

Serikali ya Tanzania imesema itawahamisha walimu wa ziada katika masomo ya sanaa kwenye shule za sekondari wapatao 7,463 kwenda shule za msingi kupunguza upungufu na kuboresha elimu hiyo ya msingi.

 Aidha, tayari majaribio ya mpango huo wa kuwahamishia walimu hao uameanza katika Mkoa wa Arusha na yakifanikiwa, itahusisha mikoa yote nchini hasa kwenye mahitaji.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Elimu, Bw. Bernard Makali alisema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati kamati hiyo ilipokuwa ikichambua taarifa za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Kamati ilikuwa inakagua taarifa hiyo kuhusu ufanisi katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi.

Makali alisema katika sekondari walimu wa sanaa (Arts) ni wengi kwa idadi hiyo ya zaidi ya 7,000 na kwamba hao wanaohamishwa wanachochea ubora wa elimu katika shule za msingi na marupurupu yao na mishahara itabaki kama ilivyo.

Kwa mujibu wa Makali, shule za msingi nchini zina upungufu wa jumla wa walimu 47,151 na ziada ya walimu wa sanaa katika shule za sekondari ni hiyo 7,463 na ndio watakaopelekwa shule za msingi.

Kuhusu upungufu wa walimu wa hisabati na sayansi, alisema wamepata kibali cha kuajiri walimu 4,129 wa masomo ya sayansi na wataalamu wa maabara.

Aidha, baadhi ya wajumbe wa kamati waliuliza kuhusu kuwepo kwa walimu wasio na sifa kazini na kutaka kujua hatua zinachukuliwa na serikali hasa baada ya kuweka utaratibu kwao kwenda kujiendeleza.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad