Serikali ya Tanzania,Rwanda na Burundi zazindua rasmi Mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo-Ngara/Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 31, 2017

Serikali ya Tanzania,Rwanda na Burundi zazindua rasmi Mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo-Ngara/Kagera.


Pichani ni Muonekano wa Daraja la Kimataifa la Rusumo lililopo wilayani Ngara mkoani Kagera linalounganisha Tanzania na Rwanda ambapo Hapo ndipo patakapo kuwa na  mradi wa umeme "Rusumo Hydro electric Power Project".


Katika mradi huo mitambo ya kufua umeme utakuwa upande wa Tanzania na kituo cha kupokea kitakuwa upande wa Rwanda eneo ambalo itaanzia miundombinu ya kusafirisha umeme.


Miundombinu ya kusafirisha umeme kwenda nchiniBurundi itapitia Tanzania upande wa Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera na itafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Serikali ya Tanzania imezindua Ujenzi wa mradi wa kufua umeme katika maporomoko ya Rusumo yaliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera ,utakaonufaisha nchi 3 za Tanzania,Rwanda na Burundi hapo Jana March 30,2017.

Uzinduzi wa mradi huo utakaogharimu dola za Kimarekani 340 milioni ,umeshuhudiwa na Mawaziri wa Nishati kutoka nchi hizo tatu sambamba na wafadhili kutoka Benki ya Dunia.

Mradi huo unatarajiwa kukamilika Februari 2020 na kuzalisha megawati 80,huku kila nchi ikipata mgawanyo  wa zaidi ya megawati 20.

Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania ,Profesa Sospeter Muhongo amesema mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia ambapo kwa upande wa Tanzania itachangia kwa asilimia mia moja.

Waziri Muhongo amebainisha kwamba ,kwa upande wa nchi ya Burundi  haitachangia gharama yoyote katika mradi huo huku nchi ya Rwanda ikichangia asilimia 50.

Ni kikundi cha wasanii kutoka Rwanda.

Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi huo-Ni kikundi cha wasanii kutoka Burundi.

Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia ,Bw.Bella Bird amesema ni miongoni mwa miradi iliyowavutia ya uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya Rusumo na hawakusita kuwekeza katika eneo hilo.

Amesema mradi huo utasaidia kuwepo kwa uhakika wa umeme katika ukanda huo na kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa nchi hizo.

Amesema mradi huo ukikamilika utapunguza mahitaji ya nishati hiyo na kufungua nafasi za ajira na kuwa Benki ya Dunia inaona kuna faida nyingi huku akisisitiza Mkandarasi wa Mradi huo kukamilisha kazi hiyo kwa mujibu wa makubaliano.

Post Bottom Ad