VPL 2016/2017:Simba SC imeilazimisha Mbeya City sare ya kufungana magoli 2-2. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Saturday, March 04, 2017

VPL 2016/2017:Simba SC imeilazimisha Mbeya City sare ya kufungana magoli 2-2.

Simba SC imeilazimisha Mbeya City sare ya kufungana magoli 2-2 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa leo March 4, 2017,kwenye uwanja wa taifa.

Mbeya City walianza kupata goli la kuongoza kipindi cha kwanza lililofungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 37 kipindi cha kwanza baada ya kuachia shuti kali kufatia kupokea pasi ya kisigino ya Raphael Daudi.


Ibrahim Ajib aliisawazishia Simba SC dakika ya 65 kipindi cha pili kwa mpira wa adhabu ndogo baada ya Mohamed Ibrahim kuangushwa nje kidogo ya box la penati. Ajibu aliuchinja mpiara na kuukwamisha kwenye nyavu huku golikipa wa Mbeya City Owen Chaima akiruka bila mafanikio.

Mbeya City hawakukata tamaa, dakika 75 Kenny Ally akaifungia Mbeya City bao la pili baada ya kugongeana pasi na Raphael Breyson ambaye alipiga pasi kwa Ditram Nchimbi aliyepiga pasi ya mwisho kwa Kenny Ally na kukwamisha mpira kambani.

Dakika zikiwa zimeyoyoma Simba SC wakapata goli la kusawazisha kwa mkwaju wa penati kufatia beki wa kushoto wa timu hiyo, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kuangushwa kwenye box.

Mkwaju wa penati ukapigwa na Shiza Ramadhani Kichuya na kuamua game hiyo kumalizika kwa sare ya kufungana 2-2.

Sare ya leo imeifanya Simba SC kuongeza pointi moja na kufikisha pointi 55 baada ya kucheza mechi 24, ipo mbele kwa pointi tatu dhidi ya Yanga SC yenye pointi 52 lakini inamchezo mmoja ambao itacheza kesho Jumapili February 4, 2017 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba SC ni mara ya pili inapata matokeo ya sare ya kufungana 2-2 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa taifa, mara ya mwisho kupata matokeo kama hayo ilikuwa ni September 21, 2013.

Post Bottom Ad