Akizungumza
baada ya viongozi hao baada kula kiapo, Rais Magufuli amewasihi waandishi wa
habari kuwa wazalendo huku akisema kuwa ikifika mahali Tanzania inaharibika,
wao pamoja na wanaowatuma juu ya nini cha kuandika pia wataharibikiwa.
Aidha,
amevikosoa baadhi ya vyombo vya habari kwa kusema kuwa, vimekua vikitoa muda
mwingi zaidi kuhusu sehemu zenye migogoro kuliko kuandika habari za maendeleo
“Kuna
vyombo vingine vya habari sehemu yenye ugomvi ndio wanapeleka kamera na habari
hizo zinapewa muda mrefu, ‘watch out.’
“Hata
magazeti ya leo ukiyaangalia, yana picha ya mtu mmoja ambaye alifanya kosa
moja, kana kwamba kosa hilo linaungwa mkono na serikali.”
Akitolea
mfano ujio wa Rais wa Benki ya Dunia nchini, Rais Magufuli alisema kuwa siku
iliyofuatia vyombo vya habari vingi havikuelezea tukio lilitokea pale Ubungo
lakini viliandika habari nyingine tofauti.
“Tunataka
kuitoa nchi katika hali ya mazoea kuipeleka katika mstari ambao ni sahihi”, alisema Rais Magufuli.
Lakini pia
alikosoa taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari ikidai kuwa Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana angezungumza na waandishi wa habari leo wakati
yeye amemtuma nchini India ambapo atakuwa huko kwa muda wa zaidi ya siku 10.
Namshukuru
Waziri Dkt Mwakyembe amekuja hapa kuapa sababu jana kwenye mitandao kuna
wengine walikuwa wakisema hatokuja kuapa, na nilikuwa nasubiri nione” alisema Rais Magufuli
HAPA
CHINI ==’’-Tazama hii Video kumsikiliza Rais Magufuli akiongea Pamoja na
walichoongea wateule wa Rais.
|
Friday, March 24, 2017
Tazama Video:Rais Magufuli na ONYO Kwa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania.
Tags
# HABARI
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment