Mabadiliko
haya yanalenga kurekebisha Muundo, Mfumo, Uongozi, Utendaji na mengineyo.
Mambo muhimu
ambayo yamezingatiwa katika marekebisho haya ni yafuatayo; –
MFUMO WA
CHAMA.
Mfumo wa
Chama, una sura ya serikali na utawala na kuwa na ngazi nyingi ya vikao vya
uamuzi. Hali hii inafanya gharama ya kukiendesha Chama kuwa kubwa, vikao
haviitishwi na maamuzi ya chama hayawafikii walengwa. Hivyo basi yafuatayo
yanazingatiwa,
Kupunguza
wingi wa vikao vya nadharia na badala yake kuwa na vikao vichache
vinavyofanyika, vyenye maamuzi yenye tija na kujenga uhai wa chama.
Kupunguza
idadi ya wajumbe au wawakilishi ili wawe wachache lakini wenye umakini na uwezo
wa kusimamia sera, itikadi, maamuzi ya chama pamoja na kuondoka urasimu na
kupunguza gharama za uendeshaji pasina kuathiri ubora wa uwakilishi.
Muundo wa
Wilaya za Chama uendane na uundo wa sasa wa wilaya za Serikali
Uzito mkubwa
umewekwa katika kuimarisha chama katika ngazi ya shina, eneo ambalo ndilo
waliko wapiga kura. Kwa kufanya hivyo, chama kitakuwa karibu na watu na
watakiona kuwa ni chama chao.
Uendeshaji
wa shughuli zote za jumuia za chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa
Chama cha Mapinduzi na Baraza la Wadhamini la Chama cha Mapinduzi.
VIONGOZI.
Viongozi
wachache wamekuwa na tabia ya kujilimbikizia nafasi nyingi za Uongozi, utendaji
na uwakilishi katika Chama na Serikali. Hali hii hushusha ufanisi na kupunguza
tija. Nafasi nyingi kwa mtu mmoja ni kushindwa kuleta ufanisi katika vikao
husika.
Hapa
imezingatiwa kuwa; ukiacha wale wanaolazimishwa kikatiba kuwa na nafasi zaidi
ya moja kwa mujibu wa mamlaka yao, kuanzia sasa nafasi za Uongozi katika chama
zitakuwa si zaidi ya moja.
KURA YA
MAONI.
Mfumo wa
kura za maoni hukusudia kuimarisha demokrasia ndani ya chama na kuashiria
nafasi ya mgombea anayeonekana kukubalika zaidi. Hata hivyo, eneo hili limekuwa
na matokeo mabaya ya kukithiri kwa rushwa na kupata viongozi wasio na imani ya
kweli ya chama wanaosaka maslahi, wafanyabiashara wenye malengo binafsi na
mamluki.
Mapendekezo
ya kuimarisha udhibiti wa kura za maoni; –
Katiba ya
CCM ya Mwaka 1977 Toleo la 2012 Ibara ya 61A(1-3) inaelekeza kura za maoni za
ubunge na uwakilishi zitapigwa kwenye mikutano mikuu ya jimbo na si kwa
wanachama wote matawini kama ilivyofanyika mwaka 2015.
Imependekezwa
ili kudhibiti taratibu za kura za maoni jimboni, kuepusha migawanyiko, kuziba
mianya ya rushwa na kuepusha wapiga kura mamluki, inapendekezwa kufanya mabadiliko
ya upigaji kura za maoni za ubunge na uwakilishi pamoja na kufuata utaratibu
ufuatao wa kuwajadili wanaogombea;
Wagombea
ubunge/uwakilishi watachukua fomu na kurudisha kwa Katibu wa CCM wa Wilaya
inayohusika. Fomu zote za wagombea ubunge/uwakilishi zitajadiliwa na kutolewa
mapendekezo katika ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa kabla ya kupigiwa kura za
maoni.
Kamati Kuu
ya Halmashauri Kuu ya Taifa itateua majina yasiyozidi matatu ambayo
yatawasilishwa mbele ya Mkutano Mkuu wa Jimbo kwa ajili ya kupigiwa kura za
maoni.
Mkutano Mkuu wa Jimbo utapiga kura za maoni kumpendekeza mwanachama
mmoja awe mgombea wa ubunge/uwakilishi katika jimbo hilo.
Mara ya
baada ya kura za maoni, mapendekezo ya uteuzi yataanzia kwenye Kamati ya Siasa
Jimbo (kwa Zanzibar), Kamati ya Siasa ya Wilaya (Tanzania Bara), Mkoa, Kamati
Maalum (Kwa Zanzibar), Kamati Kuu na hatimaye Halmashauri Kuu ya Taifa itafanya
uteuzi wa mwisho.
|
Utaratibu
huu hautawapa fursa wagombea kutengeneza makundi na kutoa rushwa kwasababu
hakuna anayejua kama atakuwepo kwenye orodha ya wagombea.
Wale wana CCM wenye
tabia ya kujiandaa na vyama zaidi ya kimoja, kwa utaratibu huu hawataweza
kujiandaa mapema kuhamia vyama vingine.
Utaratibu huu pia utasaidia kuondoa
urasimu na migawanyiko isiyokuwa na sababu.
Aidha,
utaratibu huu utahakikisha anapatikana mgombea mwenye msimamo thabiti wa Chama
na ni utaratibu halisi kwa chama kuusimamia ipasavyo.
Katika hafla
hiyo, Polepole alisema kwamba makatibu wakuu wa mikoa wa CCM walioteuliwa ni 31
ambapo 20 miongoni mwao ni wapya ambapo makatibu wa wilaya walioteuliwa ni 76 miongoni mwao ni wapya.
Baadhi ya
makatibu hao ni:
MAKATIBU
WILAYA CCM
Rehema
Ndele- Mbozi
Shaibu
Mtawa- Morogoro Vijijini
Alfred
Mwambeleko- Masasi
Said Mkoa-
Sengerema
Miriam
Kaaya- Moshi Vijijini
Agness
Msuya- Siha
Mayasa Ayoub-
Kilwa
Rafael
Maumba- Liwale
Othman
Dunga- Hanang
Nuru
Ngeleja- Chato
Clemence
Mponzi- Kilolo
Mohamed
Mfaume- Bukoba Mjini
Mwajuma
Boha- Misenyi
Hanafi
Msabaha- Kinondoni
Robert
Kelenge- Kigamboni
Martin
Mwakitabu- Chamwino
Asia
Mohameh- Chemba
Ramadhan
Dalo- Arusha
Solomoni
Itunda- Karatu
Simba
Gadafi- Longido
Amos SHimba-
Ngorongoro
MAKATIBU
MIKOA CCM.
Amina Imbo-
Ruvuma
Haula
Kachambwa- Shinyanga
Donald
Magesa- Simiyu
Janeth
Kayanda- Tabora
Allan
Kingazi- Tanga
Kulwa Omary-
Morogoro
Zakaria
Mwansasu- Mtwara
Raymond
Mwangala- Mwanza
Hosea
Mpatike- Njombe
Anastazia
Amasi- Pwani
Kajolo
Peter- Katavi
Naomi
Kapambala- Kigoma
Jonathan
Marko- Kilimanjaro
Mwanamasoud
Pazi- Lindi
Paza Mwamlima-
Manyara
Kulwa Omary-
Morogoro
Elias
Mpanda- Arusha
Jamila
Yusuf- Dodoma
Adam
Ngalawa- Geita
Christopher-
Iringa
Rahel
Degeleke- Kagera
|
No comments:
Post a Comment