Baadhi ya
Vitanda hivyo vilivyomo ndani ya Wodi ya Watoto .
Na,Abel
Daud-Globu ya Jamii Kigoma.
Wakati Serikali
ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiunga mkono juhudi zinazofanywa na
Asasi,Makanisa,Mashirika na watu binafsi,wamisionari wa kanisa la Baptist
kutoka Marekani wameunga mkono juhudi za serikali kwa kujenga jengo la wodi ya
watoto katika hospitali teule ya Manispaa ya Kigoma Ujiji lenye thamani ya
shilingi milion 420.
Mkuu wa
Wilaya ya Kigoma Samson Anga-akizindua jengo hilo ameupongeza uongozi wa kanisa
hilo na kusema kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua ili kumaliza changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya,ikiwa ni pamoja na kuwataka wakazi wa
kigoma kutumia jengo hilo vizuri na kupata huduma zitakazotolewa ili kuimalisha
afya za watoto.
Aidha akisoma
risala ya uzinduzi wa jengo hilo katibu wa Hospitali teule ya Manispaa ya
kigoma ujiji Bw.Anania Raiton ameeleza kuwa bado kuna changamoto nyingi katika
sekta ya afya,na kuongeza kuwa kama serikali itachukua hatua katika kumaliza
changamoti hizo za huduma itakayo kuwa inatolewa kwa uma,itasaidia kuokoa
maisha ya wahitaji wa matibabu.
Hata hivyo
kwa upande wao wafadhili wa jengo hilo akiwemo Dr.Larry Pepper ambaye ni
mwakilishi wa wafadhili katika hospitali ya Baptist ameeleza kuwa gharama
zilizotumika ni kubwa,hivyo ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma kutumia
huduma vizuri ikiwa ni pamoja na kuepuka kuharibu vifaa ambayo vitatumika
kutolea huduma.
Kwa upande
wake Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Baptist Kilawa Shido amesema kuwa kuwepo
sasa kwa jengo hilo,wakazi wa Kigoma watarajie kunufaika sambamba na kutoa shukurani
kwa wafadhili,huku akiitaka serikali kuongeza wahudumu katika sekta ya afya
kwani uhitaji wao ni mkubwa mno.
|
No comments:
Post a Comment