Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi
mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimian na mbunge
wa Kilwa Kaskazini Vedasto Ngombale (CUF) mara baada ya kuhutubia wananchi wa
Nangulukulu mkoani Lindi.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia msaada wa
Shilingi milioni moja kijana Abdulrahman Khalid ambaye ni mlemavu wa miguu
katika eneo la Mchinga-1 mkoani Lindi, Katikati(Mwenye shati la maua) ni Mbunge
wa Mchinga Hamidu Bobali kupitia chama cha (CUF) ambaye ameahidi kumpatia
mlemavu huyo kiasi cha Shilingi Milioni moja pia.
PICHA NA
IKULU.
Rais wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa kuwa Serikali
haitatoa chakula cha msaada kwa watakaopatwa na njaa ilihali wanaweza kuzalisha
chakula katika maeneo yao.
Rais
Magufuli ametoa kauli hiyo Jana March 02,2017 katika ziara yake mkoani Pwani, wakati
akizungumza na wananchi wa Somanga, Nangurukuru na Mchinga Moja, ikiwa ni ziara
yake katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
Amepokea
kero za wananchi katika maeneo hayo nakuwataka
kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuzalisha mazao ya chakula cha kutosha
"Najua
mmezoea kusikia maneno mazuri mazuri kuwa hakuna atakayekufa kwa njaa, sasa
mimi nasema usipofanya kazi, usipolima mazao na kupata chakula wakati mvua
inanyesha Serikali haitatoa chakula cha bure kwa wenye njaa, ni lazima tufanye
kazi, sasa hivi mvua zinanyesha limeni mazao ya chakula" amesisitiza Mhe.
Rais Magufuli.
Pia Rais
Magufuli amezungumza na wananchi wa Ikwiriri na kupokea kero zao ambapo
amewaagiza Mamlaka ya Maji katika Mji huo kuhakikisha mradi wa maji uliojengwa
na kukamilika tangu mwaka 2015 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 5, unaanza
kutoka maji kabla ya mwisho wa Mwezi huu na pia amepiga marufuku utozaji wa
ushuru kwa wafanyabiashara wadogowadogo wa mazao.
Aidha, Mhe.
Dkt. Magufuli amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Lindi kushughulikia migogoro ya
wakulima na wafugaji iliyoanza kuibuka mkoani humo na ameahidi kutoa Shilingi
Milioni 20 kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Somanga.
Mbali na
hayo Rais Magufuli amewaagiza Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
kujenga kituo cha mabasi cha Nangurukuru na pia amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa
wa Lindi kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Hamidu Bobali
kuhakikisha anapeleka Daktari katika kijiji cha Mchinga Moja ili kutatua kero
ya wananchi kukosa huduma ya matibabu.
Mhe. Rais
Magufuli ataendelea na ziara yake leo tarehe 03 Machi, 2017 hapa Mkoani Lindi
|
No comments:
Post a Comment