Hawa ndio Viongozi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa Nchini waliochaguliwa kwa Kura zote. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 29, 2017

Hawa ndio Viongozi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa Nchini waliochaguliwa kwa Kura zote.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba, ambaye kachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wakurugenzi Nchini.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Ndg Anne Claire Shija (Kushoto) ambaye kachaguliwa kuwa katibu wa Wakurugenzi nchini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA wa Wakurugenzi Nchini.

Na Mathias Canal, Dodoma.

Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kote nchini Tanzania, kwa kauli moja wameridhia na kuwachagua Viongozi watakaowawakilisha katika kufikisha changamoto zao mbalimbali katika ngazi za juu ili kupungunza uwasilishaji wa kila Mkurugenzi kufikisha changamoto zake ngazi za juu.

Uchaguzi huo umefanyika hii Leo katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma kwa maridhiano ya Wakurugenzi wote kwa asilimia 100% ya kura zote.

Uchaguzi huo umejiri Mara baada ya kumalizika kikao cha kazi kilichoongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Eng Musa Iyombe kilichohudhuriwa na Wakurugenzi wote 185.

Wakurugenzi hao wamefanya uchaguzi kwa nafasi nne ambazo ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti sambamba na Katibu Mkuu na Muweka Hazina.

Wakurugenzi waliochaguliwa katika nafasi hizo ni-

1. Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba, ambaye kachaguliwa kuwa Mwenyekiti

2. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndg Rachel Chuwa ambaye kachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.

3. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Ndg Anne Claire Shija, ambaye kachaguliwa kuwa katibu. 

Na

4. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo  Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mara baada ya uchaguzi huo kumalizika Viongozi hao waliochaguliwa wameeleza namna bora ya kuhumiza uwajibikaji kwa Wakurugenzi wote sambamba na kuwawakilisha vyema kufikisha changamoto zao kwa ngazi za juu.

Wameueleza mtandao wa www.wazo-huru.blogspotm.com kuwa imani kubwa waliyopatiwa na Wakurugenzi wote nchini ya kuwachagua kuwa wawakilishi wao ni kubwa hivyo wana kila sababu ya kuitumikia kwa weledi na usawa.

"Kupitia Wawakilishi hao waliochaguliwa Wakurugenzi nchini wataraji utendaji uliotukuka na uwakilishi unaostahili kulingana na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao" Alisema MD Kayombo John L.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad