Viongozi wakuu wa Kamati za Ulinzi na Usalama Kibondo mkoani Kigoma,Tanzania na wenzao wa Mikoa ya Chankuzo, Ruyigi, Kitega nchini Burundi wakutana katika kikao cha ujirani Mwema Nchini Burundi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 29, 2017

Viongozi wakuu wa Kamati za Ulinzi na Usalama Kibondo mkoani Kigoma,Tanzania na wenzao wa Mikoa ya Chankuzo, Ruyigi, Kitega nchini Burundi wakutana katika kikao cha ujirani Mwema Nchini Burundi.


Mkuu wa Wilaya Kibondo mkoani Kigoma nchini Tanzania, Bw.Luis Bura  kushoto pichani na Mkuu wa Usalama wa Jimbo la Ruyigi na Chankuzo nchini Burundi, Kanal Elia Ndizigiye kulia,walipokuwa katika kikao  cha ujirani Mwema Nchini Burundi.

Mkuu wa Mkoa wa Ruyigi, Bw. Abdalah Hassan mwenye kofia Nchini Burundi na Mkuu wa Wilaya Kibondo mkoani Kigoma nchini Tanzania, Bw.Luis Bura walipokuwa katika kikao  cha ujirani Mwema Nchini Burundi.

Kutokana na hali ya usalama kwenye mipaka ya nchi za Burundi na Tanzania kulegalega kwa kushamili vitendo vya uharifu wa kutumia siraha Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma nchini Tanzania imekutana na Kamati za ulinzi za mikoa ya Chankuzo, Ruyigi, Kitega nchini Burundi na kuweka mikakati  ya kuzuia uharifu huo unaoendelea kugharimu maisha ya watu na mali zao.

Akiongea katika Kikao hicho kilichofanyika March 27, 2017 Mkoani Ruyigi Nchini Burundi mkuu wa wilaya ya Kibondo Tanzania,Bw. Luis Bura alisema makundi ya uharifu yanayoonekana kuvuka mipaka na kufanya ujambazi kwa kufanya mauwaji yanakuwa ni tishio kwakuwa Watanzania hivi sasa hawafanyi kazi zao kwa amani na kuvitaka vyombo vya ulinzi pande zote kushirikina.


‘’Makundi ya waharifu wanao tumia siraha wanaonekana kuvuka mika na kuingia nchini mwetu kuuwa watu sasa mauwaji ya raia wetu sasa basi kinachotakiwa kamati zenu na serikali kwa ujumla kuliangalia kwa umakini mkubwa jambo hili maana ni hatari sana watu wet kwa sasa hawafanyi kazi zao kwa amani kwa kuhofia kuvamiwa hata mashambani hawaendi ''...alisema Bura.
 
Kwa upande wake  mkuu wa Mkoa wa Ruyigi Abdalah Hassan alisema ili kuwepo mafanikio katika vita dhidi ya uharifu lazima vyombo husika pande wajenge utaratibu wa kukutana kila mara ili kujadiri namna na kupeana taarifa za haraka  kushirikiana

Mkuu wa upelelezi wa Mkosa ya Jinai wilayani Kibondo upande wa Tanzania, Rutatinisibwa Tibyeilwa aliitaka Serikali ya Burundi kudhibiti uzagaaji wa siraha za Moto kwakuwa watu wamekuwa wakikamtwa nchini Tanzania wanapohojiwa, udai kuwa wanazinunua Burundi

Baadhi ya wajumbe wa Kamati za ulinzi na usalama Wilayani Kibondo,Mkoani Kigoma nchini Tanzania  na wenzao wa Mikoa ya Ruyigi Chankuzo na Kitega nchini Burundi walipokuwa katika kikao cha ujirani mwema.

‘’ Siaraha nyingi za Moto zimekuwa zikikamatwa  katika maeneo mengi ya nchi yetu mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Tabora, Mara, Dar Es Salaam na wahusika wanapohojiwa ueleza kuwa wanazinunua huku kwenu nchini Burundi na zimekuwa zikisababisha madhala makubwa sana hivyo tunaomba mjitahidi kudhibiti hali hiyo kwa kuwa si nzuri''... alisema Rutatinisibwa. 

Mkuu wa usalama wa Jimbo la Ruyigi na Chankuzo, Kanal Elia Ndizigiye amekieleza kikao hicho kuwa nchi ya Burundi ilipoingia katika matatizo wahasi walikimbia na siraha nyingi zikiwemo sare za jeshi hivyo hao ndo chanzo cha uzagaaji wa siraha bila utaratibu ili kudhibiti hali hiyo lazima ufanyike mkakati maalum.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad