Miradi
aliyoitembelea Bw. Rodriguez ni
pamoja na mradi wa ujenzi wa vyoo, madarasa,
mabweni na jengo la utawala katika shule ya Msingi Mgeza Mseto Manispaa
ya Bukoba ambapo mara baada ya kukamilika mradi utagharimu Dola za Kimarekani
(318,000 USD) ambapo ujenzi wa vyoo umekamilika, madarasa mabweni na jengo la
Utawala ujenzi upo katika hatua ya msingi.
Bw. Rodriguez akiongea na wanafunzi, walimu na
wananchi waliofika kumpokea katika shule hiyo alisema kuwa amefurahishwa kufika
katika shule hiyo na kujionea hali halisi ya watoto wenye ulemavu wa albinizimu
na walemavu wengine aidha, alisema kuwa Umoja wa Mataifa uliamua kutoa fedha
hizo ili kurejesha miundombinu ya shule hiyo baada ya kuharibiwa na Tetemeko la
Ardhi lilitokea Septemba 10, 2016.
“Nilipokuwa Dar es Salaam niliambiwa na Waziri
Profesa Joyce Ndalichako kuwa nikifika Kagera nitembelee Shule ya Msingi Mugeza
Mseto pia nilipofika Kagera Mkuu wa Mkoa ameniambia nitembelee shule hii sasa
nimejionea na kujua ni kwanini walinisistiza, shule inahitaji msaada mkubwa.
Aidha, Umoja wa Mataifa unapenda kusaidia lakini Tanzania shule za namna hii zipo nyingi na ndiyo maana
tunasaidia kidogo kidogo ili kuongeza mahitaji muhimu.” Alisistiza Bw. Rodriguez
|
Pai Bw. Rodriguez alisema kuwa mara baada
ya kujionea hali halisi ya shule hiyo ataendelea kushawishi wafadhili
mbalimbali ili kuhakikisha shule hiyo yenye mahitaji maalum inapewa kipaumbele
katika ufadhili.
Vilevile aliiomba jamii kutowanyanyapaa watoto wenye ulemavu
kwani ulemavu hauna ukabila, utaifa wala rangi ambapo alisema kuwa hata yeye
watoto wake ni walemavu jambo ambalo alisema ulemavu hauna mzungu wala mweusi.
Umoja wa
Maifa pia umetoa ufadhili dola za Kimarekani (250,000 USD) kwenye shule za
Msingi 16 Katika Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ili
kujenga vyoo na kuimarisha mifumo ya maji kwa ajili ya uboreshaji wa usafi na
mazingira.
Pia kukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa na Tetemeko la Ardhi
lililotokea mwaka jana 2016.
Aidha, Umoja
wa mataifa kupitia Shirika lake la (UNICEF) ulitoa ufadhili wa kujenga majiko
sanifu katika jamii kwaajili ya kutunza mazingira kwa wananchi wa hali ya chini
kwa kutumia nishati ya kuni kidogo.
Pia kupitia shirika la (IOM) wananchi na
kaya masikini waliokumbwa na Tetemeko la
Ardhi mwaka 2016 waligawiwa vifaa mbalimbali kama ndoo, magodoro, blanketi, bati, vyandarua na
vifaa vya kujengea makazi ya muda katika Halmashauri za Bukoba Manispaa, Bukoba
na Missenyi.
|
Katika Hatua
nyingine Bw. Rodriguez alikagua
mradi uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa wa kufunga umeme wa jua katika Zahanati
ya Bushasha Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Shule ya St. Mary Rubya Seminari
Wilayani Muleba. Katika Shule ya Rubya Seminari ufungaji wa umeme wa jua
uligharimu Dola za Kimarekani (50,000 USD) hadi kukamilika.
Akitoa
maelezo ya Mradi huo Padre Malianus
Rutagwerela ambaye ndiye Mkuu wa Seminari hiyo alisema kuwa mradi huo
umeongeza nguvu ya mwanga katika shule hiyo na kuwa na umeme wa uhakika ikiwa
ni pamoja na umeme wa TANESCO.
Aidha aliushukuru umoja wa Mataifa kwa niaba ya
uongozi wa Jimbo Katoliki la Bukoba kuwa mradi huo utaboresha zaidi elimu
katika Seminari hiyo.
|
Naye
Mkurugenzi Mkazi Bw. Rodriguez alifurahishwa sana na mradi huo ambao
alishuhudia ukifanya kazi vizuri.
“ Nimefurahishwa na mradi huu pia sisi kama
Umoja wa Mataifa tutaendelea kuona jinsi ya kusaidia shule kama hizi ili
Mapadre na Viongozi wa dini waendelee kuzalishwa katika shule kama hizi ili
wasaidie kueneza neno la Mungu kuhusu upendo na kuondoa chuki kati ya Wanadamu.
Alieleza Bw. Rodriguez
Mwisho, Bw.
Rodriguez alisema kuwa amefurahishwa na utekelezaji wa miradi ambayo ipo chini
ya Mashirika ya Umoja wa Maifa ambayo imetolewa ufadhili wa fedha na Umoja huo
na kutekelezwa au inaendelea kutekelezwa Mkoani Kagera.
Aidha, alihaidi kuendelea kuushawishi Umoja huo na
wafahili mbalimbali ili waendelee kuuangalia na kuufadhili Mkoa wa Kagera
katika miradi mbalimbali ya maendeleao na Kijamii.
Habari/Picha Na: Sylvester Raphael
|
No comments:
Post a Comment