VPL 2016/2017: Yanga SC yalipa kisasi cha goli 4-0 kwa Stand United . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 03, 2017

VPL 2016/2017: Yanga SC yalipa kisasi cha goli 4-0 kwa Stand United .


Mabingwa watetezi wa ligi kuu Soka Tanzania bara ,Yanga SC wameendelea kujikita kileleni mwa ligi kuu msimu huu 2016/2017  baada ya mchezo wao wa leo February 03,2017 kupata  ushindi wa nguvu wa magoli 4-0 dhidi ya Timu ya  Stand United.

Katika mchezo huo,Magoli ya Yanga SC yamefungwa na Donald Ngoma aliyeanza kufunga goli la kwanza dakika ya 18, Simon Msuva akafunga dakika ya 27 kisha Obrey Chirwa akafunga bao la tatu dakika ya 46 kabla ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kukamilisha ushindi kwa kufunga dakika ya 68.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC iendelee kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu baada ya kufikisha pointi 49 wakiwa wameshacheza mechi 21 pointi nne mbele ya watani wao wa jadi Simba SC wenye pointi 45 wakiwa wamecheza mechi 20.

Simba SC watacheza kesho Jumamosi February 04 dhidi ya Majimaji FC , kama watashinda mechi hiyo gape litaendelea kusalia pointi moja lakini matokeo ya sare yatafanya Simba SC kuwa nyuma kwa pointi tatu na wakipoteza mechi hiyo watakuwa wameachwa kwa pointi nne.

Msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya mechi ya Yanga SC vs Stand United.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad