VIDEO:Cameroon vs Ghana 2-0 ● Fainali February 05,2017 ni Misri na Cameroon. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 03, 2017

VIDEO:Cameroon vs Ghana 2-0 ● Fainali February 05,2017 ni Misri na Cameroon.

Timu ya Taifa ya Cameroon wameingia Fainali ya AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika, baada kuifunga Ghana 2-0 hapo Jana February 02, huko Nchini Gabon.

Magoli ya Cameroon yalifungwa na Michael Ngadeu dakika ya 72 kabla ya Christian Bassogog kuzima ndoto za Ghana kucheza fainali dakika za nyongeza, ushindi huo unaifanya Cameroon kutinga fainali ya AFCON 2017 na watacheza na fainali dhidi ya Misri, fainali ambayo itakuwa inajirudia ya mwaka 2008 ambapo Misri alimfunga Cameroon na kutwaa taji lake la sita.
Sasa Cameroon watacheza Fainali na Egypt hapo Jumapili kupata Bingwa wa Afrika 2017 wakati Ghana wakicheza Jumamosi na Burkina Faso kusaka Mshindi wa Tatu. 

Mshindi wa 3.

Jumamosi Februari 04,2017

2200 Burkina Faso v Ghana

Fainali

Jumapili Februari 05,2017.

2200 Egypt v Cameroon

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA.

-Egypt-Mara 7

-Cameroon, Ghana-Mara 4

-Nigeria-Mara 3

-Congo DR-Mara 2

-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1

Post Bottom Ad