VPL 2016/2017: Mavugo na Kichuya yailiza Yanga SC na Simba SC kuwa Alama 5 katika msimamo wa Ligi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 25, 2017

VPL 2016/2017: Mavugo na Kichuya yailiza Yanga SC na Simba SC kuwa Alama 5 katika msimamo wa Ligi.

Pambano la Dabi ya Kariakoo,Dar Es Salaam, likichezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Leo February 25,2017,ikiwa ni mwendelezo wa Mechi ya Ligi kuu Vodacom Tanzania bara 2016/2017,ilishuhudia Mtu 10 uwanjani,Simba SC ikitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Yanga SC bao 2-1.

 Jina la Shiza Kichuya limechukua nafasi na kuwa gumzo mjini kufuatia uwezo ambao ameonyesha katika mchezo huo wa wapinzani wa jadi, Simba SC na Yanga SC mara baada ya kutokea benchi na kuisaidia timu yake kusawazisha goli kisha yeye mwenyewe kufunga goli la pili na la ushindi.

Dakika ya 55 Simba SC walibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Janvier Besala Bokungu kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kulambwa Kadi za Njano 2.
Shiza Kichuya aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Novalty Lufunga katika dakika ya 51, wakati huo Simba ikiwa imeshatulizwa kwa goli moja lililofungwa kwa mkwaju wa penati na Simon Msuva wa Yanga SC katika dakika ya tano ya mchezo huo.

Tangu kuingia kwa Kichuya mchezo ulionekana kubadilika na mashambulizi kugeukia katika goli la Yanga SC na katika dakika ya 67 alipiga krosi ambayo ilimkuta Mrundi, Laudit Mavugo ambaye alipiga kichwa kilichoingia moja kwa moja nyavuni na mchezo kuwa ni goli moja kwa moja kwa kila upande.

Dakika 14 baadae baada ya Mavugo kusawazisha, ikiwa ni dakika ya 81, Shiza Kichuya aliwainua mashabiki wa Simba SC kwa kufunga goli la pili baada ya kupiga krosi iliyomshinda golikipa wa Yanga SC, Deo Munishi na kutinga katika nyavu ndogo ya pembeni.

Mpaka mwamuzi Mathew Akrama wa Mwanza anapuliza filimbi ya kuashiria kumalizika kwa dakika tisini za mchezo huo Simba SC ambayo ndiyo ilikuwa mwenyeji wa mchezo ikiwa na magoli mawili na Yanga SC ikiwa na goli moja.

Ushindi wa Simba SC dhidi ya watani wao wa jadi Yanga SC umewawezesha kuzidi kupaa kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa kufikisha alama 54 na kuwaacha Yanga SC kwa alama tano nyuma yao ambao wao wanazo alama 49 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Ratiba/Mat okeo:

Jumamosi Februari 25,2017

Simba 2 Yanga 1

Jumamosi Machi 04,2017

Simba v Mbeya City

Ndanda FC v Ruvu Shooting

Toto African v Mbao FC

Azam FC v Stand United

Kagera Sugar v Maji Maji FC

Jumapili Machi 05,2017

Mtibwa Sugar v Yanga

African Lyon v Mwadui FC

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad