UEFA 2016/2017: FC Barcelona wachapwa 4-0 ugenini na PSG. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, February 15, 2017

UEFA 2016/2017: FC Barcelona wachapwa 4-0 ugenini na PSG.

Huko Parc des Princes Jijini Paris Nchini France Mabingwa, Paris St Germain waliwafumua Miamba ya soka wa Uhispania FC Barcelona mabao 4-0 katika Mechi ya Kwanza ya hatua ya Mtoano ya Timu 16 ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Angel di Maria alianza kuwaandikishia PSG goli kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja hadi wavuni na katika dakika ya 40.

Katika Mechi hiyo ya PSG na Barca, Bao za PSG zilipigwa na Angel Di Maria, Dakika za 18 na 55, Julian Draxler, 40', na Edinson Cavani, 71'.
Kipigo hiki kinaiweka Barcelona pagumu kufuzu kwenda Robo Fainali na wakishindwa hilo hii itakuwa mara ya kwanza kwao kutotinga Robo Fainali katika Miaka 10.

Katika mchezo mwingine Benfica ya Ureno wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Borrrusia Dotmund ya Ujerumani kwa bao la Konstantinos Mitroglo.

Dortmund  walikosa Penati baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kupiga na Kipa Ederson kuukoa.
Ligi hiyo itaendelea tena leo Jumatano kwa michezo miwili Bayern Munich wakiwaalika Arsenal nao Real Madrid wakiwa wenyeji wa Napoli.

Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo

Mechi za Kwanza.

Jumatano 15, Februari 2017

Bayern Munich v Arsenal      
           
Real Madrid v Napoli  

Jumanne 21, Februari 2017

Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid   
           
Manchester City v Monaco       
        
Jumatano 22, Februari 2017

FC Porto v Juventus        
       
Sevilla v Leicester City           

Post Bottom Ad