Malori ya makontena yabakiza wiki 9 Dar - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, February 15, 2017

Malori ya makontena yabakiza wiki 9 Dar

Bandari Kavu (ICD) ya Ruvu mkoani Pwani, ambayo ujenzi wake unalenga kupunguza msongamano wa malori jijini Dar es Salaam, utakamilika ndani ya wiki tisa zijazo na utagharimu Sh bilioni 7.3.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema jijini Dar es Salaam jana kwamba ujenzi huo unafanywa na Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT), ambao jana walisaini mkataba wa ujenzi huo na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Profesa Mbarawa alisema mara tu ujenzi huo utakapokamilika, makontena yote yatapelekwa kwenye bandari hiyo ya Ruvu kwa reli na malori yanayotoka mikoani na nchi jirani, yatakuwa yanachukulia mizigo yao huko badala ya kuja Dar es Salaam.

Tunatarajia kuwa ujenzi ukikamilika ndani ya wiki hizo tisa, bandari hiyo itaanza kufanya kazi,” alifafanua Profesa Mbarawa.

Aliongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi huo, kutaleta ufanisi mkubwa katika bandari ya Dar es Salaam, kwa kuwa hakutakuwa tena na msongamano wa makontena.

Alisema ni mpango wa serikali kwamba bandaria kavu zote za jijini Dar es Salaam, zijengwe nje ya mji ili kupunguza msongamano wa magari.

Alisema kujengwa kwa Ruvu ICD, kutasaidia kupunguza msongamano wa magari, kwani malori yote ambayo kwa sasa yanalazimika kufika bandarini kwa ajili ya kuchukua shehena mbalimbali yatakomea Ruvu.

Alisema serikali imeamua kuwapa Suma JKT kujenga bandari hiyo, kwa kuwa wanawaamini kwamba wataufanya ndani ya muda uliopangwa na kwa ufanisi mkubwa.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad