‘’Steve Nyerere Atakuwa Amekamatwa na Upelelezi’’-Simon Sirro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 25, 2017

‘’Steve Nyerere Atakuwa Amekamatwa na Upelelezi’’-Simon Sirro.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).


Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa suala la Mchekeshaji na Mwigizaji wa Bongo Muvi, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ juu ya kukamatwa kwake kuwa hafahamu suala hilo labda litakuwa chini ya Idara ya Upelelezi kwa kuwa halijamfikia mezani kwake.

Kauli hiyo ameisema Jana February 25,2016, wakati alipoulizwa swali na wanahabari kuhusiana na taarifa zinazosambaa mitandaoni ya kuwa msanii huyo amekamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za makossa ya kimtandao.

Wakati huohuo, Kamanda Sirro amezungumza na wanahabari kuhusiana na watu  humiwa 257 waliokamatwa jijini Dar es Salaam kwa makossa ya madawa ya kulevya kwa kipindi cha Februari 16 hadi 23 mwaka huu kutokana na oparesheni iliyofanyika hadi sasa.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Alieleza kuwa, jumla ya kete 1526 za madawa ya kulevya aina ya Heroin zilikamatwa huku puli zikiwa 112 na misokoto ya Bangi 247 pamoja na pombe haramu aina ya gongo lita 372.

Post Bottom Ad