pesaaa

DSTV

Header Banner

Pitia Orodha ya Majina na Alichosema RC Makonda kuhusu jina “Philemoni Mbowe”

Leo February 8, 2017 -Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameingia kwenye awamu anayoiita ni ya pili kwa kutaja orodha ya watu ambao watahitajika kufika Polisi Central Dar es salaam kusaidia taarifa na maelezo kwenye mapambano ya kutokomeza dawa za kulevya Dar Es Salaam.

Kwenye orodha hiyo iliyosambaa mitandaoni kwenye jina namba 54 kuliandikwa Philemoni Mbowe na hivyo habari zikaanza kusambaa kwamba sio Freeman Mbowe aliyetajwa.

Jioni hii ya Leo, Paul Makonda amewaambiwa Waandishi wa habari kwamba jina la kwanza kwenye namba 54 lilikosewa na inatakiwa kuandikwa Freeman Mbowe hivyo anaehitajika Ijumaa ni Mheshimiwa Freeman Mbowe