Mbowe Kuendelea Kutokamatwa na Polisi Wala Kuwekwa Kizuizini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 23, 2017

Mbowe Kuendelea Kutokamatwa na Polisi Wala Kuwekwa Kizuizini.

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameongea na waandishi wa habari jioni hii  baada ya kutoka Mahakamani  kwenye kesi iliyofunguliwa na Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa Mkoa w Dar Paul Makonda  na Kamshna Sirro.

Lissu amesema Amri ya kuzuia Freeman Mbowe asikamatwe na wala kuwekwa kizuizini na Polisi inaendelea isipokua wanaweza kumuita kwa Mahojiano ambapo pia Mahakama itatoa maamuzi Tarehe 2, March  2017
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene  amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu.
Wema pamoja mama yake, leo aliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho kwenye mahakama kuu jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo aliyeshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad