Arsenal dhidi ya Bayern Munich, "Walisambaratika Kiakili" - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 16, 2017

Arsenal dhidi ya Bayern Munich, "Walisambaratika Kiakili"

Arsenal "walisambaratika kiakili" wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya hatua ya 16 bora mikononi mwa Bayern Munich, meneja Arsene Wenger amesema.

Gunners walilazwa goli 5-1 katika mechi iliyochezwa huko Allianz Arena Jijini Munich Nchini Germany.

"Ni vigumu kueleza," Wenger aliambia BT Sport.
"Muda mfupi kabla ya mapumziko, tulikuwa na nafasi mbili nzuri za kufunga. Tulirejea na kucheza vyema.

"Kipindi cha pili, tulimpoteza Koscielny upesi - alitoka tukiwa 1-1 - na hatimaye tukasambaratika. Bayern ni timu nzuri kutushinda vpia.

"Nilihisi bao la tatu liliangamiza wachezaji wetu kabisa kwa sababu baada ya hapo hatukuweza kujibu tena.
Lakini Kipindi cha Pili, ndani ya Dakika 20, Bayern walifunga Bao 3 za chapchap kupitia Robert Lewandowski na Thiago Alcantara, na kuongoza 4-1.

Dakika ya 88, Thomas Muller akaipa Bayern bao lao la 5 na kupata ushindi mnono wa 5-1 kwa kuisambaratisha Timu ya Arsene Wenger.

Hii inawaweka hatarini ya kuondolewa tena hatua ya muondoano kwa msimu wa saba mtawalia.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad